Mkutano wa tisa wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika wafanyika Beijing

(CRI Online) Septemba 04, 2024

Chinese Foreign Minister Wang Yi, also a member of the Political Bureau of the Communist Party of China Central Committee, addresses the Ninth Ministerial Conference of the Forum on China-Africa Cooperation (FOCAC) in Beijing, capital of China, Sept. 3, 2024.

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi akihutubia Mkutano wa tisa wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika mjini Beijing, China, Septemba 3, 2024. (Xinhua/Zhang Ling) 

Mkutano wa tisa wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ulifanyika jana hapa Beijing, ambao umefanya maandalizi ya pande zote kwa mkutano wa kilele wa Baraza hilo unaoanza leo Septemba 4.

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema, kauli mbiu ya mkutano huo wa kilele ni “Kushirikiana kuelekea kuwa nchi za mambo ya kisasa, na kujenga kwa pamoja jumuiya ya kiwango cha juu ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja”, ambayo inafuata matakwa ya lazima ya maendeleo ya historia na kuonesha matarajio ya pamoja ya watu wa China na Afrika. Ameongeza kuwa, rais Xi Jinping wa China atashirikiana na viongozi wa nchi za Afrika kuweka mpango mpya wa uhusiano kati ya China na Afrika, na kuelekeza mwelekeo wa maendeleo ya nchi za kusini.

The Ninth Ministerial Conference of the Forum on China-Africa Cooperation (FOCAC) is held in Beijing, capital of China, Sept. 3, 2024. (Xinhua/Li Xiang)

Mkutano wa tisa wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ukifanyika Beijing, China, Septemba 3, 2024. (Xinhua/Li Xiang)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha