Mkutano wa Pili wa Baraza la Indonesia na Afrika wakamilika mjini Bali, Indonesia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 04, 2024

Picha hii iliyopigwa Septemba 3, 2024 ikionyesha mkutano na waandishi wa habari wa kufungwa kwa Mkutano wa 2 wa Baraza la Indonesia na Afrika (IAF) huko Bali, Indonesia. (Xinhua/Xu Qin)

Picha hii iliyopigwa Septemba 3, 2024 ikionyesha mkutano na waandishi wa habari wa kufungwa kwa Mkutano wa 2 wa Baraza la Indonesia na Afrika (IAF) huko Bali, Indonesia. (Xinhua/Xu Qin)

BALI, Indonesia – Mkutano wa Pili wa Baraza la Indonesia na Afrika (IAF) lenye kaulimbiu ya "Moyo wa Bandung kwa Agenda ya Afrika 2063," ambao umekutanisha wajumbe zaidi ya 1,400 kutoka nchi 29, wakiwemo wakuu saba wa nchi za Asia na Afrika, pamoja na mawaziri, wajasiriamali na wasomi, ambalo lilifanyika kuanzia Jumapili huko Bali, Indonesia, limehitimishwa jana Jumanne.

Baraza hilo limejikita katika kuimarisha ushirikiano kati ya Indonesia na nchi za Afrika katika sekta muhimu za nishati, usalama wa chakula, afya na madini.

Dewi Justicia Meidiwaty, Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Indonesia, amesema siku ya Jumanne kwamba baraza hilo limeimarisha uhusiano wa kiuchumi kwa mafanikio kati ya Indonesia na nchi za Afrika kwani limetumika kama sehemu ya kimkakati kwa mashirika ya serikali, kampuni za kitaifa, kampuni za kibinafsi, pamoja na kampuni za wastani, ndogo na za kati kuanzisha ushirikiano wa kunufaishana na washirika kutoka Afrika.

"IAF 2024 linatarajiwa kuongeza ukuaji wa uchumi na kuimarisha msimamo wa Indonesia katika ngazi ya kimataifa kupitia mikataba mbalimbali iliyotiwa saini," amesema Meidiwaty.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Indonesia Retno Marsudi amesisitiza mafanikio ya baraza hilo kwenye mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatatu. Amebainisha kuwa mikataba ya biashara yenye thamani ya dola bilioni 3.5 za Kimarekani imesainiwa kwenye mkutano huo, ikiwa ni ongezeko kubwa kutoka dola za Kimarekani milioni 586.6 zilizosainiwa katika mkutano wa kwanza wa IAF Mwaka 2018.

Pia ametangaza kuwa Indonesia itakuwa mwenyeji wa Jubilee ya Platinamu ya Mkutano wa Asia na Afrika Mwaka 2025, kuadhimisha miaka 70 tangu kufanyika kwa mkutano huo wa kihistoria.

Mgeni akipiga picha katika ukumbi mkuu wa Mkutano wa 2 wa Baraza la Indonesia na Afrika (IAF) mjini Bali, Indonesia, Septemba 3, 2024. (Xinhua/Xu Qin)

Mgeni akipiga picha katika ukumbi mkuu wa Mkutano wa 2 wa Baraza la Indonesia na Afrika (IAF) mjini Bali, Indonesia, Septemba 3, 2024. (Xinhua/Xu Qin)

Picha hii iliyopigwa Septemba 3, 2024 ikionyesha ukumbi mkuu wa Mkutano wa 2 wa Baraza la Indonesia na Afrika (IAF) mjini Bali, Indonesia. (Xinhua/Xu Qin)

Picha hii iliyopigwa Septemba 3, 2024 ikionyesha ukumbi mkuu wa Mkutano wa 2 wa Baraza la Indonesia na Afrika (IAF) mjini Bali, Indonesia. (Xinhua/Xu Qin)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha