Biashara kati ya Afrika na China inakua kwa kasi

(CRI Online) Septemba 04, 2024

Takwimu zilizotolewa na Idara kuu ya Forodha ya China zimeonyesha kuwa, China imeendelea kuimarisha biashara na nchi za Afrika katika miaka ya karibuni, huku kukiwa na ongezeko kubwa la biashara kati ya pande hizo mbili.

Takwimu zilizotolewa na Idara Kuu ya Forodha ya China zimeonesha kuwa, kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka jana, thamani ya biashara kati ya China na Afrika iliongezeka kwa dola za kimarekani bilioni 28 kutoka chini ya dola za kimarekani milioni 14.08, na iliongezeka kwa asilimia 17.2 kuliko mwaka uliopita.

Katika kipindi cha mwezi Januari hadi Julai mwaka huu, biashara kati ya China na Afrika iliongezeka kwa asilimia 5.5 na kufikia kiwango cha juu katika historia ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

China imejikita kwa muda mrefu katika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na nchi za Afrika, na uhusiano wa kiviwanda kati ya pande hizo mbili umeendelea kuwa wa karibu zaidi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha