Wataalamu na maofisa wakutana nchini Kenya kwa lengo la kuboresha huduma ya afya kanda ya Afrika Mashariki

(CRI Online) Septemba 05, 2024

Watalamu na maofisa wamekutana jijini Nairobi, Kenya, kujadili njia za kuboresha upatikanaji wa huduma za afya katika kanda ya Afrika Mashariki.

Mkutano huo wa siku tatu wa Maonyesha ya Tiba ya Afrika Mashariki umekutanisha zaidi ya wageni 8,000, washiriki 200, na maofisa waandamizi wa serikali, wakuu wa mahospitali na wahudumu wa afya kutoka zaidi ya nchi 30, ambao wanatafiti njia za kuongeza uvumbuzi katika sekta ya afya ya kanda hiyo.

Katibu mkuu wa Wizara ya Afya ya Kenya Mary Muriuki amesema, nchi nyingi za Afrika Mashariki zinakabiliwa na changamoto nyingi za kiafya kwa kuwa hazijatimiza lengo la Umoja wa Afrika la kutumia asilimia 15 ya bajeti zao katika sekta ya afya.

Rais wa Shirikisho la Teknolojia ya Maabara ya Matibabu nchini Uganda Patrick Alibu ameitaka kanda ya Afrika Mashariki kutimiza upatikanaji wa huduma za afya kwa wote, hususan kwa watu wa vijijini na wenye mapato ya chini wanaoishi mijini.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha