Rais wa Comoro asema mawasiliano kati ya Afrika na China ni mfano wa ushirikiano katika "Dunia ya Kusini"

(CRI Online) Septemba 05, 2024

Rais wa Comoro Bw. Azali Assoumani amesema, katika ushirikiano na nchi za Afrika, China siku zote imekuwa ikifuata kanuni za kutendeana kwa usawa na kushirikiana kwa mafanikio bila kujali ukubwa wa nchi, jambo ambalo limeweka msingi wa ushirikiano kati ya nchi za 'Dunia ya Kusini' na kuwezesha kujenga dunia ya haki ambayo maslahi ya pande zote yanalindwa.

Rais Azali amesema, katika miongo kadhaa iliyopita, China daima imefuata kanuni ya kutoingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine, na imejenga ushirikiano wenye manufaa na nchi za Afrika katika nyanja nyingi ikiwemo siasa, jamii, uchumi na maisha ya watu.

Rais Azali ameeleza matumani ya kujenga jumuiya ya ngazi ya juu ya Afrika na China yenye hatma ya pamoja katika siku zijazo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha