Marais wa China na Rwanda watangaza kuinua hadhi ya uhusiano wa pande mbili

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 06, 2024

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais wa Rwanda Paul Kagame, ambaye yuko Beijing  kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa  Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Septemba 5, 2024 (Xinhua/Yao Dawei)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping siku ya Alhamisi alikutana na Rais wa Rwanda Paul Kagame, ambaye yuko Beijing kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ambapo viongozi hao wawili wametangaza kuinua hadhi ya uhusiano wa pande mbili kuwa uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati wa pande zote.

Rais Xi amesema China inaiunga mkono Rwanda katika kufuata njia ya maendeleo ya kujitawala na kujiamulia, na inapenda kuzidisha mabadilishano ya uzoefu kuhusu utawala wa chama na nchi.

China inapenda kuongeza hali ya kuaminiana kisiasa, kupanua matarajio ya pamoja, na kuendeleza kwa pamoja ujenzi wa mambo ya kisasa na Rwanda, amesema Xi.

Amesema China inapenda kushirikiana na Rwanda kutekeleza pamoja matokeo ya mkutano wa kilele wa FOCAC wa mwaka huu, kuimarisha ushirikiano katika sekta za miundombinu, kilimo na matumizi ya satalaiti, na kusimamia pamoja kwa mafanikio Chuo cha Confucius katika Chuo Kikuu cha Rwanda na Karakana ya Luban.

Rais Xi amesema kuwa China inathamini mchango mkubwa wa Rwanda katika kudumisha amani na usalama barani Afrika na inapenda kuzidisha ushirikiano na Rwanda katika ulinzi wa amani na nyanja nyinginezo.

Kwa upande wake Kagame ameelezea shukrani zake kwa mchango muhimu wa Rais Xi katika kuhimiza amani na usalama barani Afrika, kuimarisha mshikamano na ushirikiano wa Afrika, na kuzidisha urafiki na ushirikiano kati ya Afrika na China.

Amesema Rwanda inapenda kuimarisha mabadilishano ya uzoefu kuhusu utawala wa nchi na China, kuendeleza ushirikiano wa matokeo halisi katika sekta mbalimbali, na kutekeleza kwa pamoja mapendekezo matatu kwa Dunia yaliyotolewa na Rais Xi.

Pande hizo mbili zimetoa taarifa ya pamoja kuhusu utekelezaji wa mapendekezo hayo matatu kwa Dunia.

Kwenye mkutano huo, pande hizo mbili zilitia saini nyaraka kadhaa za ushirikiano wa pande mbili katika maeneo ya utekelezaji wa Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, uuzaji wa asali nchini China, upashanaji habari na mawasiliano ya habari, pamoja na mambo ya vyombo vya habari.

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais wa Rwanda Paul Kagame, ambaye yuko Beijing  kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa  Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), kwenye Jumba la Mikutano ya Umma  la Beijing, Septemba 5, 2024 (Xinhua/Yao Dawei)

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Rais wa Rwanda Paul Kagame, ambaye yuko Beijing kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Septemba 5, 2024 (Xinhua/Yao Dawei)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha