Rais Xi Jinping apendekeza hatua za ushirikiano ili kuendeleza kwa pamoja ujenzi wa mambo ya kisasa na Afrika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 06, 2024

Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba yenye kichwa cha "Kuungana Mikono Kuendeleza Mambo ya Kisasa na Kujenga Jumuiya yenye Mustakabali wa Pamoja" wakati akihudhuria ufunguzi wa Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Septemba 5, 2024. (Xinhua/Yao Dawei)

BEIJING - China na Afrika zimekuwa na uhusiano wa karibu zaidi katika harakati zao za kujenga mambo ya kisasa wakati ambapo Rais Xi Jinping wa China katika hotuba yake kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) siku ya Alhamisi mjini Beijing ametangaza kupandisha uhusiano kati ya China na Afrika na hatua 10 za ushirikiano.

Rais Xi amependekeza kuwa uhusiano wa pande mbili kati ya China na nchi zote za Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia na China upandishwe kuwa uhusiano wa kimkakati.

Pia amependekeza uhusiano kati ya China na Afrika kuinuliwa kuwa jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja ya hali zote katika zama mpya.

Dira ya Ujenzi wa Mambo ya Kisasa kwa Nchi za Kusini

Rais Xi amesisitiza kuwa kujenga mambo ya kisasa ni "haki isiyoweza kuondolewa kwa nchi zote", akisema hakutakuwa na Dunia ya kisasa bila ya China na Afrika yenye mambo ya kisasa.

Amesema juhudi za pamoja za kujenga kwa pamoja mambo ya kisasa za China na Afrika zitaibua wimbi la kujenga mambo ya kisasa katika Nchi za Kusini na kufungua ukurasa mpya wa kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu.

Hotuba hiyo ya Rais Xi imepongezwa na viongozi waliohudhuria mkutano huo akiwemo Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Guterres amesema ushirikiano kati ya China na Afrika ni nguzo kuu ya ushirikiano wa Kusini na Kusini.

"Maendeleo yenye kasi ya ajabu ya China, ikiwa ni pamoja na kutokomeza umaskini, yanatoa tajiriba ya uzoefu na utaalamu mwingi. Afrika inaweza kutumia kikamilifu faida za uungaji mkono wa China katika maeneo ya biashara, mambo ya fedha na teknolojia," amesema Guterres.

Hatua za ushirikiano halisi

Ili kutimiza maono ya kujenga mambo ya kisasa, Rais Xi amependekeza hatua 10 za ushirikiano ziweze kutekelezwa katika miaka mitatu ijayo, ambazo zinahusu kufunzana kati ya ustaarabu, ustawi wa biashara, ushirikiano wa mnyororo wa viwanda, mafungamano ya mawasiliano, ushirikiano wa maendeleo, afya, kilimo, mawasiliano kati ya watu na ya kitamaduni, maendeleo ya kijani na usalama wa pamoja.

Azimio la kujenga kwa pamoja jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja ya hali zote kwa zama mpya na mpango kazi wa FOCAC kwa miaka mitatu ijayo umepitishwa siku hiyo ya Alhamisi kwenye mkutano huo.

Hatua mpya za kivitendo zilizotangazwa na Rais Xi ni uthibitisho zaidi wa ahadi yake ya mara kwa mara ya kuinua ushirikiano kati ya China na Afrika kwa ngazi za juu zaidi, amesema Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye. 

Rais Xi Jinping wa China na viongozi wa kigeni wakipiga picha ya pamoja kabla ya hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Septemba 5, 2024. (Xinhua/Rao Aimin)

Rais Xi Jinping wa China na viongozi wa kigeni wakiwasili kuhudhuria hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Septemba 5, 2024. (Xinhua/Yin Bogu)

Rais Xi Jinping wa China na viongozi wa kigeni wakiwasili kuhudhuria hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Septemba 5, 2024. (Xinhua/Yan Yan)

Rais Xi Jinping wa China na viongozi wa kigeni wakihudhuria ufunguzi wa Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Septemba 5, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Rais Xi Jinping wa China na viongozi wa kigeni wakiwasili wakihudhuria ufunguzi wa Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Septemba 5, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Rais Xi Jinping wa China na viongozi wa kigeni wakihudhuria ufunguzi wa Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kwenye Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, China, Septemba 5, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha