China kutoa Msamaha wa Ushuru kwa Bidhaa Zote kutoka kwa Nchi zilizoko nyuma kimaendeleo (LDCs) Kuanzia Desemba 1, 2024

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 13, 2024

Ofisi ya Kamati ya Ushuru ya Baraza la Serikali la China tarehe 12 imesema kuwa, kamati hiyo imetoa tangazo hivi karibuni, ikisema ili kupanua ufunguaji mlango kwa nchi zilizoko nyuma kimaendeleo(LDCs) na kutimiza maendeleo kwa pamoja, kuanzia Desemba 1, 2024, China itasamehe ushuru kwa bidhaa zote zinazozalishwa katika nchi zilizoko nyuma kimaendeleo ambazo zina uhusiano wa kidiplomasia na China.

Katika bidhaa hizo, kwa bidhaa ambazo zimetengwa mgao maalumu wa kutozwa ushuru nafuu, ushuru wa mgao huo utapunguzwa hadi sifuri, lakini ushuru wa bidhaa nyingine utaendelea kubaki kama ulivyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha