Treni za chini ya ardhi za Beijing zawezesha malipo ya moja kwa moja kwa kutumia kadi za benki za kigeni

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 14, 2024

Septemba 13, James Patrick kutoka Canada akitumia kadi za benki za kigeni kuingia treni za chini ya ardhi kwenye Kituo cha Xinshougangyuan. (Xinhua/Zhang Chenlin)

Septemba 13, James Patrick kutoka Canada akitumia kadi za benki za kigeni kuingia treni za chini ya ardhi kwenye Kituo cha Xinshougangyuan. (Xinhua/Zhang Chenlin)

Beijing imekuwa mji wa kwanza katika bara la China kuwezesha malipo ya Treni za chini ya ardhi ya moja kwa moja kwa kutumia kadi za benki za kigeni.

Kuanzia Ijumaa, watalii wa kimataifa wanaweza kutumia kadi za MasterCard na Visa zinazotolewa katika nchi za nje ili kupanda treni za chini ya ardhi katika mtandao mzima wa usafiri wa treni ya chini ya ardhi mjini Beijing, na kulipa kiotomatiki kwa malipo sawa na wakazi wa nchini.

Kamati ya Mawasiliano ya Usafiri ya Beijing ilitangaza katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Huduma ya 2024 ya China yanayofanyika hapa Beijing kuwa, imeboresha vifaa zaidi 20,000 katika mfumo wake wa treni za chini ya ardhi ili kuwezesha hatua mpya ya malipo, na kuboresha zaidi uzoefu wa watalii wa kimataifa wanapopanda treni za chini ya ardhi.

Kuanzia Januari hadi Julai mwaka huu, Beijing ilihudumia watalii milioni 1.995, ikiongezeka kwa asilimia 227.9 kuliko kipindi kama hicho mwaka uliopita. Kwa kurahisisha utaratibu wa biashara na kurekebisha vikomo vya idadi ya malipo, idadi na thamani ya malipo kwa simu yaliyofanywa na wageni mjini Beijing katika robo ya pili zimeongezeka maradufu kuliko robo ya kwanza ya mwaka huu.

Septemba 13, mtalii mmoja akitumia kadi za benki za kigeni kupanda treni za chini ya ardhi kwenye Kituo cha Xinshougangyuan. (Xinhua/Zhang Chenlin)

Septemba 13, mtalii mmoja akitumia kadi za benki za kigeni kupanda treni za chini ya ardhi kwenye Kituo cha Xinshougangyuan. (Xinhua/Zhang Chenlin)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha