China yakaribisha washirika wengi zaidi wa nchi za Kusini kujiunga na BRICS

(CRI Online) Septemba 14, 2024

Mkurugenzi wa Ofisi ya mambo ya nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Bw. Wang Yi hivi karibuni alisema, China inakaribisha washiriki wengi zaidi wenye nia moja kutoka nchi za Kusini kujiunga na familia ya BRICS.

Kwenye mazungumzo kati ya wawakilishi waandamizi wanaoshughulikia mambo ya usalama wa BRICS na nchi za Kusini, Bw. Wang alisema nchi za BRICS na nchi za Kusini zina maslahi ya pamoja katika pande nyingi. Ameongeza kuwa China inaziunga mkono nchi za BRICS kufungua mlango wa ushirikiano, na kukaribisha washiriki wengi zaidi kujiunga na familia ya BRICS, ili kuhimiza maendeleo ya uwazi, usimamizi wa dunia na maelewano kati ya nchi zenye ustaarabu tofauti, na kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha