Mauzo ya mazao ya kilimo cha bustani nchini Kenya yashuka kwa asilimia 3.5 katika nusu ya kwanza ya mwaka huu

(CRI Online) Septemba 18, 2024

Kwa mujibu wa takwimu mpya za kiuchumi zilizotolewa Jumanne na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Kenya (KNBS) mjini Nairobi, mapato ya Kenya yanayotokana na mauzo ya nje ya mazao ya kilimo cha bustani yamepungua kwa asilimia 3.5 katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, kutokana na kupungua kwa mauzo ya nje kwenye masoko ya Ulaya na Asia.

KNBS imesema, nchi hiyo imepata shilingi bilioni 86.8 (dola za Kimarekani takriban milioni 673) katika kipindi hicho, ikiwa ni chini kutoka dola milioni 697 katika kipindi kama hicho mwaka 2023.

Katika miezi sita ya kwanza ya 2024, Kenya iliuza nje tani 214,676 za maua, matunda na mboga, ikiwa ni punguo kutoka tani 291,118 katika kipindi kama hicho mwaka 2023.

Kupungua kwa mapato katika nusu ya kwanza ya mwaka huu kumechangiwa kwa kiasi fulani na kuimarika kwa shilingi ya Kenya, ambayo imefanya mauzo ya nje kuwa ghali zaidi na kupunguza mahitaji.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha