Mkuu wa majeshi ya Israel: Israel inaharakisha maandalizi ya operesheni ya ardhini nchini Lebanon

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 26, 2024

Picha hii iliyopigwa Septemba 25, 2024 ikionyesha moshi ukifuka kupaa angani kufuatia shambulizi la anga la Israel huko Khiam, Lebanon. (Picha na Taher Abu Hamdan/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Septemba 25, 2024 ikionyesha moshi ukifuka kupaa angani kufuatia shambulizi la anga la Israel huko Khiam, Lebanon. (Picha na Taher Abu Hamdan/Xinhua)

JERUSALEM - Israel inaharakisha maandalizi ya mashambulizi ya ardhini dhidi ya Hezbollah, mkuu wa majeshi ya Israel, Herzi Halevi amesema siku ya Jumatano, ikiwa ni siku ya tatu ya mashambulizi makali zaidi ya Israel dhidi ya Lebanon kuwahi kufanywa tangu Mwaka 2006.

"Mnasikia ndege zikiruka juu ... tumekuwa tukishambulia siku nzima, ili kuandaa mazingira yenye uwezekano wenu wa kuingia (nchini Lebanon) na kuendelea kuipunguza makali Hezbollah," Halevi amewaambia wanajeshi wa Kikosi cha 7 cha Kivita kwenye mazoezi karibu na mpaka wa Israel na Lebanon.

Kauli yake hiyo imetangazwa baada ya taarifa ya Hezbollah mapema siku hiyo ya Jumatano kwamba imepanua eneo lake la mashambulizi na kurusha kombora la balestiki kushambulia makao makuu ya shirika la kijasusi la Israel, Mossad, kaskazini mwa Tel Aviv. Kombora hilo lilizuiliwa, lakini Halevi ameonya kwamba Hezbollah itakabiliwa na "ulipizaji mkali sana," akiwataka wanajeshi "kujitayarisha."

Halevi amesisitiza kuwa hakutakuwa na kulegea katika operesheni ya kijeshi ya Israel iliyoanza Jumatatu. "Hatukomi," amesema, huku akisisitiza kuwa Israel inajiandaa kuingia katika vijiji vya Lebanon.

"Buti zenu za kijeshi zitaingia katika eneo la adui, na kuingia katika vijiji ambavyo Hezbollah imetayarisha kuwa vituo vikubwa vya kijeshi vyenye miundombinu ya chini ya ardhi, vituo vya kuweka silaha, na kurushia makombora (kwa ajili ya mashambulizi) katika eneo letu," amewaambia makamanda. "Mtaingia ndani, angamizeni adui huko, na bomoeni kabisa miundombinu yao."

Lengo, Halevi amesema, ni kuweka mazingira kwa wakaazi waliokimbia makazi yao kurejea makwao kaskazini mwa Israel, ambako kushambuliana kunakovuka mpaka na Hezbollah kumeongezeka tangu Oktoba mwaka jana, sambamba na vita kati ya Israel na Hamas katika Ukanda wa Gaza.

Tokeo Jumatatu wiki hii, Israel imekuwa ikifanya mashambulizi makubwa zaidi nchini Lebanon kuwahi kutokea tangu Mwaka 2006, yakisababisha vifo vya watu zaidi ya 550 na majeruhi zaidi ya 1,835 nchini kote. Mashambulizi hayo pia yamefanya wakaazi wengi kukimbia makazi yao.

Kuongezeka huko kwa kasi kwa mapigano kumeibua wasiwasi kuhusu uwezekano wa vita kamili kati ya Israel na Hezbollah, huku kukiwa na hofu kwamba mataifa mengine ya kikanda yenye nguvu pia yanaweza kuingizwa kwenye vita hivyo.

Madaktari wakitoa matibabu kwa mvulana aliyejeruhiwa huko Tripoli, Lebanon, Septemba 25, 2024. (Picha na Khaled Habashiti/Xinhua)

Madaktari wakitoa matibabu kwa mvulana aliyejeruhiwa huko Tripoli, Lebanon, Septemba 25, 2024. (Picha na Khaled Habashiti/Xinhua)

Picha hii ikionyesha moshi uliosababishwa na shambulizi la Israeli huko Marjeyoun, Lebanon, Septemba 23, 2024. (Picha na Ali Hashisho/Xinhua)

Picha hii ikionyesha moshi uliosababishwa na shambulizi la Israeli huko Marjeyoun, Lebanon, Septemba 23, 2024. (Picha na Ali Hashisho/Xinhua)

Mfumo wa kuzuia makombora wa Israeli ukirusha makombora ili kuzuia roketi zilizorushwa kutoka Lebanon, kama inavyoonekana kutoka Haifa, kaskazini mwa Israel, Septemba 24, 2024. (Picha na Jamal Awad/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha