Umoja wa Afrika wasisitiza haja ya kufanyia mageuzi mifumo ya elimu barani Afrika

(CRI Online) Septemba 27, 2024

Umoja wa Afrika (AU) umesisitiza haja ya kufanyia mageuzi mifumo ya elimu barani Afrika kuelekea kutoka elimu bora na ambayo ni yenye kuhimili mazingira mbalimbali kwa wote.

Taarifa iliyotolewa na Umoja huo imesema, kauli hiyo imetolewa kwenye mkutano uliofanyika Jumatano chini ya kaulimbiu ya “Kuwekeza katika Kesho: Mwaka wa Elimu wa Umoja wa Afrika Unaochochea Maendeleo kwa Afrika na Dunia.”

Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat amesisitiza haja muhimu ya kuhakikisha upatikanaji wa elimu bora kwa Waafrika wote, huku lengo kuu likiwa ni katika makundi yaliyo katika mazingira hatarishi zaidi, hususan wasichana na watu wenye ulemavu.

Kuhusu sekta ya elimu barani Afrika kuathiriwa na ukosefu wa usalama unaotokana na mapigano, Bw. Mahamat ametoa wito wa ulinzi wa taasisi za elimu na kusisitiza kuwa elimu inapaswa kutumika kuwa mwanga wa matumaini na injini ya maendeleo.

Aliyekuwa Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ambaye pia ni mwenyekiti wa Bodi ya Ushirikiano wa Dunia kwa ajili ya Elimu, amesisitiza kuwa kuwekeza katika elimu ni uwekezaji unaohakikisha hatma nzuri kwa Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha