Maofisa wa serikali na taasisi za kimataifa watoa wito wa kuimarisha usimamizi wa data barani Afrika

(CRI Online) Septemba 29, 2024

Maofisa kutoka serikalini na taasisi za kimataifa wametoa wito wa kuongezeka kwa matumizi ya data katika utungaji sera, wakisisitiza umuhimu wa kutumia maarifa yanayotokana na data ili kuhimiza ufanyaji maamuzi bora katika sekta mbalimbali.

Wito huo umetolewa kwenye hafla ya ufunguzi wa Kongamano la pili la Afrika Vumbua (Innovate Africa) lililofanyika mjini Kigali.

Mkurugenzi wa Takwimu katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Bw. Samson Babatunde Omotosho amesema bila ya usimamizi mzuri wa data, kutakuwa na upungufu mwingi unaoweza kufanya utungaji sera kuwa mgumu na kudhoofisha imani katika mifumo ya serikali.

Bw. Omotosho amesisitiza kuwa umuhimu kuongeza ushirikiano thabiti kati ya watayarishaji na watumiaji wa data, akisema kuwa uwekezaji mkubwa katika ukusanyaji na uchambuzi wa takwimu hautakuwa na maana kama hautachangia kwenye utungaji sera, kwani hautaleta mchango halisi kwa maisha ya watu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha