China yalaani msaada wa kijeshi wa Marekani ulioidhinishwa kwa eneo la Taiwan

(CRI Online) Oktoba 01, 2024

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lin Jian amesema msaada wa kijeshi wa Marekani kwa eneo la la China la Taiwan, bila kujali kiasi chake, hautayumbisha azma ya China ya kupinga kile kinachoitwa " Uhuru wa Taiwan" na kulinda mamlaka ya taifa na ukamilifu wa ardhi ya China.

Msemaji huyo ameyasema hayo kufuatia taarifa iliyochapishwa kwenye tovuti ya Ikulu ya Marekani inayotangaza uamuzi wa Marekani wa kutoa msaada wa kijeshi kwa eneo hilo la Taiwan wenye thamani ya karibu dola za kimarekani milioni 567.

Akijibu swali kwenye mkutano na wanahabari, Bw. Lin amesema kulipatia silaha eneo hilo la Taiwan, Marekani kwa mara nyingine imekiuka kwa kiasi kikubwa kanuni ya kuwepo kwa China moja na taarifa tatu za China na Marekani, na hasa Taarifa ya Pamoja ya Agosti 17.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha