Lugha Nyingine
Rwanda yatoa miongozo ya kudhibiti mlipuko wa Marburg
Wizara ya afya ya Rwanda imetangaza miongozo mipya ya kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa virusi vya Marburg (MVD) baada ya idadi ya watu waliofariki kutokana na ugonjwa huo kuongezeka hadi kufika watu wanane.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na wizara hiyo siku ya Jumapili, watu 26 wamethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo na kati yao 18 wamewekwa karantini na kupewa matibabu. Wizara hiyo imewataka raia kuepuka kukutana kwa karibu na watu wenye dalili za ugonjwa huo, ikiwemo homa kali, maumivu makali ya kichwa na misuli, kutapika na kuhara.
Vituo vyote vya afya vimetakiwa kufuata kwa makini hatua za kinga na udhibiti wa maambukizi wakati wa kushughulikia wagonjwa wenye dalili za ugonjwa huo. Pia Wizara hiyo imetaka idadi ya watu wanaohudhuria mazishi ya waliofariki kwa ugonjwa huo isizidi 50.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma