Mjumbe wa kudumu wa China ahimiza kuziunga mkono nchi za Maziwa Makuu katika kuimarisha mshikamano na ushirikiano

(CRI Online) Oktoba 09, 2024

Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Fu Cong amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuziunga mkono nchi za Maziwa Makuu katika kuimarisha mshikamano na ushirikiano, na kujenga mustakabali wa pamoja.

Fu Cong ameyasema hayo siku ya Jumanne, aliposhiriki kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya masuala ya eneo la Maziwa Makuu, akisema kuwa katika siku za hivi karibuni, nchi za Maziwa Makuu zimekuwa zikiweka jitihada katika kutafuta amani, usalama na maendeleo, na kuwa chachu kubwa katika kustawisha Mfumo wa Amani, Usalama na Ushirikiano wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na eneo la Maziwa Makuu.

Ameongeza kuwa wakati huohuo, eneo hilo bado linakabiliwa na changamoto mbalimbali, kama vile vurugu zinazoendelea na janga kubwa la kibinadamu.

Ametoa wito kwa nchi za kikanda kuimarisha mazungumzo na maafikiano, kushikilia kuishi pamoja kwa amani, kukabiliana na changamoto kwa pamoja, kudumisha usalama wa pamoja, kupunguza janga la kibinadamu, na kuhimiza maendeleo ya pamoja.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha