China inatazamia kuendeleza urafiki wa jadi, ushirikiano na Thailand: Waziri Mkuu Li

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 11, 2024

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Waziri Mkuu wa Thailand Paetongtarn Shinawatra pembezoni mwa mikutano ya viongozi kuhusu ushirikiano wa Asia Mashariki iliyofanyika Vientiane, Laos, Oktoba 10, 2024. (Xinhua/Zhang Ling)

VIENTIANE - Waziri Mkuu wa China Li Qiang alipokutana na mwenzake wa Thailand Paetongtarn Shinawatra pembezoni mwa mikutano ya viongozi kuhusu ushirikiano wa Asia Mashariki mjini Vientiane, Laos amesema China ingependa kushirikiana na Thailand kutumia maadhimisho ya mwakani ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kama fursa ya kuendeleza zaidi urafiki wa jadi, kuimarisha mawasiliano ya kimkakati, kuendeleza ushirikiano na kusukuma mbele ujenzi wa jumuiya ya China na Thailand yenye mustakabali wa pamoja.

China na Thailand ni marafiki wa karibu na majirani wanaounganishwa na milima na mito, Li amesema, akiongeza kuwa chini ya mwongozo wa kimkakati wa viongozi wa nchi hizo mbili, ujenzi wa jumuiya ya China na Thailand yenye mustakabali wa pamoja umeendelea kusonga mbele, ukiwa na ushirikiano wenye mafanikio katika nyanja mbalimbali na mawasiliano kati ya watu yaliyo motomoto.

Dhana ya "China na Thailand kama familia moja" imepata umaarufu mkubwa, ameongeza.

Amesema kuwa inatarajiwa kuwezesha uhusiano kati ya China na Thailand kuwa karibu zaidi na kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi hizo mbili.

Li amesema kuwa China inaunga mkono kithabiti Thailand katika kufuata njia ya maendeleo inayoendana na hali yake ya kitaifa, na ina nia daima ya kuwa mshirika wa kuaminika na wa kutegemeka wa Thailand.

Waziri Mkuu wa China pia ametoa wito kwa pande hizo mbili kuandaa kwa pamoja shughuli za kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia mwaka ujao na kuimarisha mabadilishano katika vyombo vya habari, utamaduni, utalii, elimu na vijana ili kuimarisha uungaji mkono wa umma kwa urafiki kati ya nchi hizo mbili.

Kwa upande wake, Paetongtarn ametoa pongezi za dhati kwa maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, akieleza imani thabiti kwamba chini ya uongozi wa Rais Xi Jinping, China itaendelea kuwa na nguvu zaidi na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa amani na ustawi wa Dunia.

Akisema kuwa mwaka ujao ni maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Thailand na China, Paetongtarn amesema Thailand ina nia ya kuandaa kwa pamoja mfululizo wa sherehe na China, kuimarisha zaidi mawasiliano ya ngazi ya juu na kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana katika nyanja mbalimbali.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Waziri Mkuu wa Thailand Paetongtarn Shinawatra pembezoni mwa mikutano ya viongozi kuhusu ushirikiano wa Asia Mashariki iliyofanyika Vientiane, Laos, Oktoba 10, 2024. (Xinhua/Zhang Ling)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Waziri Mkuu wa Thailand Paetongtarn Shinawatra pembezoni mwa mikutano ya viongozi kuhusu ushirikiano wa Asia Mashariki iliyofanyika Vientiane, Laos, Oktoba 10, 2024. (Xinhua/Zhang Ling)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha