Mwandishi wa vitabu wa Jamhuri ya Korea Han Kang ashinda Tuzo ya Nobel ya Fasihi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 11, 2024

Katibu Mkuu wa Taasisi ya Sayansi ya Sweden, Mats Malm akitangaza mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi Mwaka 2024 mjini Stockholm, Sweden, Oktoba 10, 2024. (Xinhua/Peng Ziyang)

Katibu Mkuu wa Akademia ya Sweden, Mats Malm akitangaza mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi Mwaka 2024 mjini Stockholm, Sweden, Oktoba 10, 2024. (Xinhua/Peng Ziyang)

STOCKHOLM - Mwandishi wa vitabu wa Jamhuri ya Korea Han Kang ametunukiwa Tuzo ya Nobel ya Fasihi ya Mwaka 2024, Akademia ya Sweden imetangaza jana Alhamisi na kumfanya Han kuwa mwandishi wa vitabu wa kwanza wa Jamhuri ya Korea kushinda tuzo hiyo ya kifahari.

Taasisi hiyo imemsifu "kwa nathari zake kali za kishairi ambazo zinakabili kiwewe cha kihistoria na kufichua udhaifu wa maisha ya binadamu."

Anders Olsson, mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Nobel ya Fasihi, amepongeza "huruma ya kimwili ya Han kwa walio katika mazingira hatarishi, huwa ni maisha ya wanawake" ya wahusika wake.

"Ana ufahamu wa kipekee juu ya uhusiano kati ya mwili na roho, walio hai na wafu, na kwa mtindo wa kishairi na majaribio, amekuwa mvumbuzi katika nathari ya zama tulizonazo," Olsson amesema.

Riwaya yake "The Vegetarian" (Mtu asiyekula nyama), ambayo ilishinda Tuzo ya Kimataifa ya Booker Mwaka 2016, inaendelea kuwa kazi yake inayotambuliwa duniani. Pia ameandika kazi vitabu vingine vinavyosifiwa kama vile Matendo ya Binadamu, Kitabu Cheupe, na Masomo ya Kigiriki.

Katibu Mkuu wa  Taasisi ya Sayansi ya Sweden, Mats Malm akitangaza mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi Mwaka 2024 mjini Stockholm, Sweden, Oktoba 10, 2024. (Xinhua/Peng Ziyang)

Katibu Mkuu wa Akademia ya Sweden, Mats Malm akitangaza mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi Mwaka 2024 mjini Stockholm, Sweden, Oktoba 10, 2024. (Xinhua/Peng Ziyang)

Katibu Mkuu wa Taasisi ya Sayansi ya Sweden, Mats Malm akitangaza mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi Mwaka 2024 mjini Stockholm, Sweden, Oktoba 10, 2024. (Xinhua/Peng Ziyang)

Katibu Mkuu wa Akademia ya Sweden, Mats Malm akitangaza mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi Mwaka 2024 mjini Stockholm, Sweden, Oktoba 10, 2024. (Xinhua/Peng Ziyang)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha