

Lugha Nyingine
China ingependa kushirikiana na Laos katika kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya ngazi ya juu: Waziri Mkuu wa China
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi ya Watu wa Laos na Rais wa Lao Thongloun Sisoulith mjini Vientiane, Laos, Oktoba 11, 2024. (Xinhua/Liu Bin)
VIENTIANE - Waziri Mkuu wa China Li Qiang siku ya Ijumaa alipokutana na Thongloun Sisoulith, katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi cha Laos ambaye pia ni Rais wa Laos amesema kuwa China ingependa kushirikiana na Laos kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kwenye kiwango cha juu, ubora wa juu, na ngazi ya juu na kuleta manufaa zaidi kwa watu wa nchi hizo mbili.
Akiwasilisha salamu za upendo kutoka kwa Xi Jinping, katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ambaye pia ni Rais wa China, kwa Thongloun, Li ameipongeza Laos kwa kuandaa kwa mafanikio mfululizo wa mikutano ya viongozi kuhusu ushirikiano wa Asia Mashariki.
China na Laos ni makomredi na ndugu wa kijamaa, Li amesema, akiongeza kuwa katika miaka 60 iliyopita tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, uhusiano kati ya vyama na nchi hizo mbili umehimili changamoto za mabadiliko katika nyanja ya kimataifa na kuonyesha uhai mpya.
Katibu Mkuu Xi na Katibu Mkuu Thongloun wamedumisha mawasiliano ya karibu ya kimkakati kati yao ili kuongoza ujenzi wa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya kati ya China na Laos, amesema Waziri Mkuu huyo.
Amesema kuwa China inaiunga mkono kithabiti Laos katika kufuata njia ya kijamaa inayoendana na hali halisi ya nchi yake na ingependa kuendelea kuungana mkono kithabiti katika masuala yanayohusu maslahi ya kimsingi na mambo yanayofuatiliwa ya kila mmoja.
Kwa upande wake Thongloun amemwomba Li kufikisha salamu zake za dhati kwa Rais Xi. Amepongeza mafanikio ya mkutano wa tatu wa wajumbe wote wa kamati kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China, pamoja na maadhimisho ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China.
Akipongeza mafanikio ya kihistoria ya maendeleo ya China na kuongezeka kwa ushawishi wake kimataifa chini ya uongozi thabiti wa Kamati Kuu ya CPC huku Komredi Xi Jinping akiwa kiongozi wake mkuu, Thongloun amesema chama, serikali na watu wa Laos wamekuwa wakiichukulia China kama jirani asiyekuwa na mbadala, rafiki mzuri, komredi mzuri na mshirika mzuri.
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi ya Watu wa Laos na Rais wa Lao Thongloun Sisoulith mjini Vientiane, Laos, Oktoba 11, 2024. (Xinhua/Liu Bin)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma