Kuifahamu China | kufafanua Ujenzi wa Mambo ya Kisasa wa China ulio wa binadamu kuishi pamoja na mazingira ya asili katika hali ya kupatana

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 15, 2024

"Jambo muhimu la kuifahamu China, ni kufahamu Ujenzi wa Mambo ya Kisasa wa China."

Tovuti ya Gazeti la Umma (People’s Daily Online) sasa imetoa vipindi vipya vinavyoitwa "Kuifahamu China", ambavyo vinafafanua na kuwasilisha picha halisi na ya pande zote ya China kupitia mazungumzo ya kina kati ya viongozi wa siasa wa nchi mbalimbali na wasomi wa ndani na nje ya China.

Ujenzi wa Mambo ya Kisasa wa China ni njia ya kujenga Mambo ya Kisasa kwa watu bilioni 1.4. Kutimiza binadamu kuishi pamoja na mazingira ya asili katika hali ya kupatana ni sifa wazi ya Ujenzi wa Mambo ya Kisasa wa China.

Katika kipindi hiki cha "Kuifahamu China",Wang Yuanfeng, mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti wa teknolojia na mkakati vya uwiano sawa wa kaboni katika Chuo Kikuu cha Mawasiliano cha Beijing, pamoja na Patrick Nijs, Balozi wa zamani wa Ubelgiji nchini China walifanya mazungumzo wakichambua hali tofauti na ya kufanana kati ya China na Magharibi katika dhana ya maendeleo ya ikolojia, pamoja na ufunuo kwa Dunia uliotokana na ujenzi wa mambo ya kisasa wa China ulio wa binadamu kuishi pamoja na mazingira ya asili katika hali ya kupatana.

Patrick Nijs alisema, nchi za magharibi hazipaswi kuhangaikia katika nafasi zake za uongozi, bali zinapaswa kukubali mabadiliko katika muundo wa dunia, na kushirikiana na nchi zinazojitokeza ili kutimiza hali ya uwiano wa dunia nzima.

Wang Yuanfeng alisisitiza, baada ya China kutoa wazo la “Ujenzi wa Ustaarabu wa Mazingira ya Ikolojia ”, imetoa hatua za mfululizo ili kutekeleza mpango wa jumla wa uhifadhi wa mazingira ya ikolojia na maendeleo ya uchumi. Alisema kuwa ujenzi wa mambo ya kisasa wa China ulio wa binadamu kuishi pamoja na mazingira ya asili katika hali ya kupatana unaweza kutoa mfano kwa nchi zote duniani,na kutoa mchango kwa pamoja kwa ajili ya maendeleo ya ikolojia ya dunia.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha