Goldman Sachs yapandisha makadirio yake ya ukuaji wa uchumi wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 15, 2024

Mtu akifahamishwa kuhusu ndege isiyoendeshwa na rubani katika Eneo la Vyombo vya Usafiri vya Teknolojia za Kisasa kwenye Maonyesho ya tatu ya Kimataifa ya Biashara ya Kidijitali mjini Hangzhou, Mkoani Zhejiang, Mashariki mwa China, Septemba 25, 2024. (Xinhua/Huang Zongzhi)

NEW YORK – Benki ya Uwekezaji ya Goldman Sachs imepandisha juu makadirio yake kuhusu ukuaji wa uchumi wa China kwa Mwaka 2024 na 2025 siku ya Jumapili juu ya msingi wa hatua zilizochukuliwa hivi karibuni na China kwa ajili ya kuunga mkono ukuaji wa uchumi.

Pato la Taifa la China (GDP) litaongezeka kwa asilimia 4.9 Mwaka 2024, kutoka makadirio ya awali ya asilimia 4.7, ripoti ya benki hiyo imeeleza.

Wakati huo huo, Goldman Sachs imekadiria kuwa uchumi wa China utakua kwa asilimia 4.7 mwaka ujao, kutoka makadirio ya awali ya asilimia 4.3.

"Hatua mpya za kuchochea uchumi za China zinaonyesha wazi kuwa watunga sera wamebadili mwelekeo kuhusu usimamizi wa sera za mzunguko na kuongeza ufuatiliaji wao kwenye uchumi," wamesema wanauchumi na Goldman Sachs.

China ilipata asilimia 5.2 ya ukuaji wa Pato la Taifa Mwaka 2023 na kuweka lengo la ukuaji wa uchumi la karibu asilimia 5 kwa Mwaka 2024.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha