

Lugha Nyingine
Safaricom Yapanua Jukwaa la Malipo ya M-Pesa Kimataifa hadi Nchini Ethiopia
Wakenya sasa wataweza kutuma pesa kwenda Ethiopia kwa kutumia M-Pesa kupitia Safaricom Kenya na tawi lake la Ethiopia baada ya kampuni hiyo kupanua hudum zake kupitia huduma ya M-Pesa Global.
Upanuzi wa huduma hiyo ya M-Pesa Global unalenga kuongeza matumizi ya pesa za kielektroniki nchini Ethiopia, hivyo kusaidia uchumi wa taifa hilo na mataifa mengine ya Bara la Afrika.
Esther Waititu, Afisa Mkuu wa Huduma za Fedha wa Safaricom Kenya, amesema kwamba ushirikiano huo unadhihirisha dhamira yao ya kutoa suluhu za kifedha pamoja na huduma zinazokidhi mahitaji yanayobadilika ya wateja wao kibiashara.
Huduma hii itapatikana kwenye pochi ya M-Pesa na kwa wateja wote wa Safaricom nchini Ethiopia kupitia Utumaji Pesa Nyumbani wa Kimataifa wa M-Pesa (M-Pesa International Remittance)
Kwa kuongeza, wateja wa M-Pesa wanaweza kutuma na kupokea pesa katika nchi zaidi ya 190.
Elsa Muzzolini, Afisa Mkuu wa Huduma za Fedha wa Safaricom Ethiopia, ameongeza kwamba ushirikiano huo utawezesha wateja wa M-Pesa Ethiopia kupokea matangazo salama na ya gharama nafuu kutoka Kenya, hivyo kuongeza matumizi ya malipo ya kidijitali katika eneo hilo.
Wataalam wa masuala ya fedha wanasema hatua hiyo ni muhimu kwani itasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha uchumi na biashara baina ya Kenya na Ethiopia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma