China yaitaka Marekani kuacha kufanya mashambulizi ya mtandaoni duniani

(CRI Online) Oktoba 15, 2024

Ripoti ya pamoja iliyotolewa na Kituo cha Taifa cha Kukabiliana na Dharura ya Virusi vya Kompyuta cha China, Maabara ya Taifa ya Uhandisi wa Teknolojia ya Kuzuia Virusi vya Kompyuta, na Kampuni ya 360 imesema Marekani imetoa taarifa zisizo sahihi kwa shirika la "Volt Typhoon" na kuficha mashambulizi yake ya mtandao kwa kupata matope nchi nyingine.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bibi Mao Ning jana Jumatatu kwenye mkutano na waandishi wa habari amesema, mashirika husika ya China yametoa ripoti mbili hapo awali zilizofichua kwamba "Volt Typhoon" ni programu ya kompyuta ya utapeli ambayo inatumiwa na mashirika ya kijasusi ya Marekani na kampuni za usalama za mtandao kueneza habari zisizo za kweli kuhusu China ili kupata fungu la bajeti ya serikali. .

Bibi Mao amesema China inalaani kitendo hicho cha Marekani cha kutowajibika ipasavyo na kuitaka nchi hiyo kuacha mara moja kufanya mashambulizi ya mtandaoni duniani na kuacha kutumia masuala ya usalama wa mtandao kuichafua China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha