China ingependa kushirikiana na Kyrgyzstan ili kuimarisha hali ya kuungana mkono - Waziri Mkuu Li

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 16, 2024

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Waziri Mkuu wa Kyrgyzstan Akylbek Zhaparov pembezoni mwa Mkutano wa 23 wa Baraza la Wakuu wa Serikali za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai mjini Islamabad, Pakistan, Oktoba 15, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)

ISLAMABAD - Waziri Mkuu wa China Li Qiang alipokutana na Waziri Mkuu wa Kyrgyz Akylbek Zhaparov pembezoni mwa Mkutano wa 23 wa Baraza la Wakuu wa Serikali za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai mjini Islamabad, Pakistan siku ya Jumanne, amesema kwamba China itashirikiana na Kyrgyzstan ili kuimarisha hali ya kuungana mkono, kuendelea kuwa washirika wanaoaminiana na kutegemeana katika maendeleo na ustawi, na kuzidisha ushirikiano wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja.

Li ametaja mkutano kati ya Rais Xi Jinping wa China na Rais wa Kyrgyzstan Sadyr Japarov mjini Astana mwezi Julai, ambao uliweka mipango na utaratibu wa kujenga jumuiya ya karibu ya China na Kyrgyzstan yenye mustakabali wa pamoja na kuinua uhusiano na ushirikiano wa pande mbili hadi ngazi ya juu zaidi.

Waziri Mkuu huyo amesema China inatarajia kuimarisha uratibu na ushirikiano na Kyrgyzstan chini ya mwongozo wa kimkakati wa wakuu wa nchi hizo mbili ili kuimarisha na kuzidisha ushirikiano wa pande mbili katika nyanja mbalimbali, na kuhimiza zaidi maendeleo na ustawi wa pamoja.

Li amesema China inapenda kushirikiana na Kyrgyzstan kuweka na kuendeleza uhusiano wa pande mbili kutoka kwenye mtazamo wa kimkakati na wa muda mrefu, kuongeza zaidi mafungamano ya mawasiliano, kuharakisha kuboresha miundombinu kama vile bandari, kuhimiza biashara na uwekezaji, na kupanua ushirikiano katika sekta kama vile nishati mpya, biashara ya mtandaoni ya kuvuka mipaka, data kubwa, na akili bandia, zikijitahidi kupata matokeo mengi zaidi halisi ya ushirikiano.

Kwa upande wake, Zhaparov amesema Kyrgyzstan na China kwa muda mrefu zimekuwa majirani wa kirafiki, zikidumisha mawasiliano ya karibu ya ngazi ya juu na ushirikiano wa kunufaishana wa kiuchumi na kibiashara. Ameishukuru China kuunga mkono na kutoa msaada katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Kyrgyzstan.

Akisema kuwa Kyrgyzstan inaweka mkazo sana kwenye uhusiano kati yake na China, Zhaparov amesema kuwa Kyrgyzstan inatarajia kushirikiana na China ili kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Waziri Mkuu wa Kyrgyzstan Akylbek Zhaparov pembezoni mwa Mkutano wa 23 wa Baraza la Wakuu wa Serikali za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai mjini Islamabad, Pakistan, Oktoba 15, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akikutana na Waziri Mkuu wa Kyrgyzstan Akylbek Zhaparov pembezoni mwa Mkutano wa 23 wa Baraza la Wakuu wa Serikali za Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai mjini Islamabad, Pakistan, Oktoba 15, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha