Maofisa watoa wito wa juhudi za pamoja kushughulikia matatizo ya amani na usalama barani Afrika

(CRI Online) Oktoba 16, 2024

Wataalamu na watunga sera wamezitaka nchi za Afrika kuliweka bara hilo kuwa nguvu muhimu ya kimataifa ili kukabiliana na changamoto zilizopo na zinazoibukia za amani na usalama.

Wito huo umetolewa kwenye mkutano wa siku tatu wa mawaziri wa ulinzi wa Afrika, ulioanza Oktoba 15 mjini Addis Ababa, Ethiopia, chini ya kaulimbiu "Afrika: Kuungana katika Amani, Imara katika Usalama."

Kamishna wa Umoja wa Afrika (AU) anayeshughulikia Masuala ya Siasa, Amani na Usalama Bw. Bankole Adeoye amesema, Bara la Afrika linaendelea kukumbwa na migogoro na ukosefu wa usalama unaoathiri maisha ya mamilioni ya Waafrika.

Amesema hatari hizo za amani na usalama zinasababisha matishio mbalimbali barani Afrika, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watu wasio na makazi, ukiukwaji wa haki za binadamu, ukiukwaji wa sheria na utulivu, pamoja na hali ya kutisha ya mabadiliko ya serikali yasiyofuata katiba.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha