Watu zaidi ya 1,500 nchini Tanzania wapata matibabu bila malipo kwenye kliniki ya timu ya madaktari wa China

(CRI Online) Oktoba 16, 2024

Kundi la 27 la Timu ya Madaktari wa China nchini Tanzania imetoa matibabu bila malipo katika kliniki ya bila malipo mkoani Njombe, ambapo zaidi ya watu 1,500 wamepata huduma za matibabu.

Madaktari hao wametoa huduma katika kliniki hiyo iliyopewa jina la “Ushirikiano wa Afya Unainufaisha Tanzania” mkoani Njombe kuanzia tarehe 9 hadi 12 mwezi huu, na huduma hizo zilijumuisha upasuaji, macho, upasuaji wa neva, na tiba ya magonjwa ya moyo.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka amewashukuru madaktari hao wa China kwa kutoa huduma za bila malipo za uchunguzi, tiba na dawa kwa wakazi wa mkoa huo.

Balozi wa China nchini Tanzania, Chen Mingjian alizindua rasmi kliniki hiyo ya bila malipo, na kueleza mafanikio ya timu hiyo ya madaktari wa China nchini Tanzania kwa mwaka mmoja uliopita, na kufafanua mafanikio ya ushirikiano kati ya China na Tanzania katika sekta ya afya.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha