China iko tayari kuimarisha ushirikiano na pande zote katika usalama wa chakula

(CRI Online) Oktoba 17, 2024

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bibi Mao Ning amesema, China iko tayari kuendelea kuimarisha ushirikiano na pande zote katika usalama wa chakula na kujenga kwa pamoja dunia isiyo na njaa.

Msemaji huyo ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali kuhusu Siku ya Chakula Duniani, ambayo huadhimishwa kila mwaka Tarehe 16 Oktoba na kwa mwaka huu kauli mbiu yake ni "Haki ya vyakula kwa maisha bora na mustakabali bora,”.

Msemaji huyo pia amesema China inaweka mkazo mkubwa katika suala la usalama wa chakula duniani, na kutoa msaada wa dharura wa chakula kwa nchi zinazokumbwa na maafa ya asili na migogoro ya kibinadamu, na kubadilishana uzoefu na teknolojia za kilimo, ili kusaidia nchi zinazoendelea kuboresha uwezo wao wa uzalishaji wa chakula.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha