Uhusiano Imara kati ya Marekani na China ni muhimu kwa amani, ustawi ya dunia: Hafla ya NCUSCR

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 17, 2024

Rais wa NCUSCR Stephen Orlins akizungumza kwenye Hafla ya kila mwaka ya Kamati ya Taifa ya Uhusiano kati ya Marekani na China (NCUSCR) mjini New York, Marekani, Oktoba 15, 2024. (Xinhua/Li Rui)

Rais wa NCUSCR Stephen Orlins akizungumza kwenye Hafla ya kila mwaka ya Kamati ya Taifa ya Uhusiano kati ya Marekani na China (NCUSCR) mjini New York, Marekani, Oktoba 15, 2024. (Xinhua/Li Rui)

NEW YORK – Ushirikiano wa kiujenzi kati ya Marekani na China ni muhimu siyo tu kwa nchi hizo mbili bali kwa utulivu na ustawi wa Dunia, wamesema viongozi wa kampuni na wa kidiplomasia katika Hafla ya Chakula cha Jioni ya kila mwaka ya Kamati ya Taifa ya Uhusiano kati ya Marekani na China (NCUSCR) iliyofanyika Jumanne mjini New York.

Rais wa NCUSCR Stephen Orlins ameongoza hafla hiyo akikiri hali ngumu ya sasa ya uhusiano kati ya Marekani na China: "Nimefanyia kazi kwenye uhusiano huu kwa miaka 50, na sikumbuki wakati ambapo ulikuwa na hali mbaya sana."

Akisisitiza hitaji la ustahimilivu, Orlins amemnukuu mwanafalsafa Confucius akisema, "Katika nyakati ngumu, tunahitaji kukumbatia mawazo mapana na ustahimilivu, kubeba majukumu yetu, na kufanya bidii maradufu ili kusonga mbele kwa uthabiti kwenye njia yetu ya uhusiano kati ya Marekani na China ambao unaifanya dunia kuwa mahali salama na yenye ustawi zaidi kwa vizazi vijavyo."

Evan G. Greenberg, Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Chubb, amesisitiza mambo husika katika kusimamia uhusiano kati ya Marekani na China katika hotuba yake.

Mambo ya diplomasia na ushirikiano wa hivi karibuni kati ya serikali ya nchi hizo mbili vimetuliza kwa kiwango kikubwa kwani mawasiliano yameboreshwa, hali ambayo ni muhimu katika kudhibiti migogoro inayoweza kutokea, amesema.

"Ushirikiano kati ya watu wetu, kwa upana, ndani na nje ya serikali katika ngazi zote ni muhimu, (ikiwa ni pamoja na) biashara, wanafunzi, walimu, majopo ya washauri bingwa, wakulima," amesema Greenberg.

"Najua sote tuna maslahi ya pamoja katika kutafuta njia chanya zaidi kwa ajili ya kusukuma mbele uhusiano kati ya Marekani na China kwa kutumia njia yenye ufanisi na utulivu," ameongeza.

Evan G. Greenberg, Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bima ya Chubb akizungumza kwenye Hafla ya kila mwaka ya Kamati ya Taifa ya Uhusiano kati ya Marekani na China (NCUSCR) mjini New York, Marekani, Oktoba 15, 2024. (Xinhua/Li Rui)

William Ford (kwenye mimbari na skrini), Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya General Atlantic, ambaye pia ni mgeni wa heshima wa shughuli hiyo, akizungumza kwenye Hafla ya kila mwaka ya Kamati ya Taifa ya Uhusiano kati ya Marekani na China (NCUSCR) mjini New York, Marekani, Oktoba 15, 2024. (Xinhua/Li Rui)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Renato Lu)

Picha