Lugha Nyingine
Ushirikiano wa BRICS uliopanuliwa kutoa mchango mkubwa zaidi katika usimamizi wa dunia, asema mjumbe wa China
Washiriki wa Baraza la BRICS juu ya Ushirikiano kuhusu Mapinduzi Mapya ya Viwanda 2024 wakiwa kwenye picha ya kundi mjini Xiamen, Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China, Septemba 10, 2024. (Xinhua/Lin Shanchuan)
MOSCOW - Ushirikiano uliopanuliwa wa BRICS utatoa mchango mkubwa zaidi katika kuboresha mfumo wa usimamizi wa dunia, amesema Balozi wa China nchini Russia Zhang Hanhui katika mahojiano maalum na Shirika la Habari la China, Xinhua kabla ya Mkutano wa 16 wa Viongozi wa BRICS uliopangwa kuanza leo Oktoba 22 hadi 24 mjini Kazan, Russia akisema kuwa mkutano huo ni wa kwanza kwa viongozi wa BRICS kufanyika nje ya mtandao tangu upanuzi wa kundi hilo.
Wakati mfumo wa BRICS unapoingia katika zama mpya ya ushirikiano mkubwa zaidi, nchi wanachama wa BRICS zitaendelea kutafuta ujenzi wa mambo ya kisasa pamoja, kutoa mchango mkubwa zaidi katika kuboresha mfumo wa usimamizi wa dunia, na kutoa "suluhu za BRICS" kwenye mageuzi makubwa yanayotokea duniani kote, Zhang amesema.
Huku akibainisha kuwa nchi wanachama wa BRICS zinawakilisha kuchomoza kwa pamoja kwa masoko yanayoibukia na mataifa yanayoendelea, Zhang amesema BRICS sasa imekuwa imara, yenye ushawishi, na iliyojaa uwezo zaidi wa kifursa kwa upanuzi wake wa hivi karibuni.
"China itaendelea kufanya kazi kwa karibu na nchi wanachama wengine wa BRICS ili kuunda ushirikiano wa kiwango cha juu ulio wa pande zote, wa karibu, wenye matokeo halisi, na jumuishi, na kwa pamoja kuanza safari mpya ya BRICS," amesema.
Akisema kuwa China na Russia, zote ni nchi wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na masoko makubwa yanayoibukia, Zhang amesema nchi hizo mbili zimeshirikiana bega kwa bega, zikifanya kazi kwa karibu kutetea kithabiti mfumo wa kimataifa unaoweka umuhimu kwa Umoja wa Mataifa, matokeo ya Vita Kuu vya Pili vya Dunia, vilevile haki na usawa wa kimataifa.
Katika mkutano huo wa BRICS, Rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Russia wanatarajiwa kufanya majadiliano ya kina kuhusu uhusiano wa pande mbili, ushirikiano katika nyanja mbalimbali, na masuala makubwa ya kimataifa na kikanda, wakihimiza maendeleo imara na ya muda mrefu ya uhusiano wa pande mbili katika zama mpya, amesema.
Balozi huyo amesema, diplomasia ya wakuu wa nchi ndiyo dira na kitu kinachoimarisha uhusiano kati ya China na Russia, ikitoa mchango muhimu na wa kimaamuzi katika kuongoza mwelekeo wa uhusiano wa pande mbili.
Picha ya angani iliyopigwa Juni 17, 2022 ikionyesha jengo la makao makuu ya Benki Mpya ya Maendeleo (NDB), inayojulikana pia kwa jina la Benki ya BRICS, mjini Shanghai, mashariki mwa China. (Xinhua/Fang Zhe)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma