Vijana wa Ethiopia wamaliza mafunzo ya kuendeleza vipaji yaliyotolewa na China

(CRI Online) Oktoba 22, 2024

Vijana 102 wa Ethiopia wamehitimu mafunzo chini ya programu ya mafunzo wa China inayolenga kuwezesha wenyeji kupitia mfumo kamili wa kuendeleza vipaji.

Programu hiyo ya kujenga uwezo ya muda wa mwezi mmoja ni mpango wa Kampuni ya Uhandisi wa Barabara ya China (CFHEC), ambayo inatoa ujuzi wa kitaalamu na kiufundi kwenye masuala ya ujenzi wa majengo, ukaguzi, upimaji wa vifaa vya ujenzi na ukarabati wa mitambo.

Hafla maalum imefanyika kuashiria kukamilika kwa programu hiyo mbele ya maofisa waandamizi wa serikali ya Ethiopia, wanadiplomasia wa China, wawakilishi kutoka Taasisi ya Mafunzo ya Ufundi na Ufundi Stadi ya Ethiopia na wanafunzi.

Wanafunzi hao wameishukuru kampuni hiyo ya China kwa kuwapatia mafunzo hayo, na kusema watatumia ujuzi waliopata kwa ajili ya maendeleo ya nchi yao.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Deng Jie)

Picha