Kampuni ya China yaanza ujenzi wa barabara ya Neno-Ligowe nchini Malawi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 22, 2024

Picha hii iliyopigwa Oktoba 18, 2024 ikionyesha hafla kuanzisha ujenzi wa barabara ya Neno-Ligowe katika Wilaya ya Neno, Malawi. (Kundi la 20 la Kampuni za Reli za China/kupitia Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Oktoba 18, 2024 ikionyesha hafla kuanzisha ujenzi wa barabara ya Neno-Ligowe katika Wilaya ya Neno, Malawi. (Kundi la 20 la Kampuni za Reli za China/kupitia Xinhua)

NENO, Malawi - Kundi la 20 la Kampuni za Reli za China (CR20), pamoja na viongozi wa Malawi, wametangaza kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Neno-Ligowe katika Kijiji cha Ligowe cha Neno, mojawapo ya wilaya zilizo pembezoni za Malawi ambapo wilaya hiyo iliyo kwenye mpaka na Msumbiji kusini mwa Malawi, inajulikana kwa ardhi yake ya milima na barabara mbovu, ambazo hazipitiki wakati wa msimu wa mvua.

Afisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Neno Brightone Mphinga amesema, barabara hiyo ya Neno-Ligowe yenye urefu wa kilomita 20 ni muhimu kwa wakazi wa Neno kwani si tu itarahisisha usafirishaji wa watu na bidhaa, hasa mazao ya kilimo, bali pia itaboresha huduma za afya na elimu katika eneo hilo.

Mphinga ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua siku ya Ijumaa kuwa kampuni ya CR20 kutangaza kuanza kwa mradi huo ni hakikisho kwamba barabara hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu sasa itakamilika.

Amesema kuwa ubovu wa barabara hiyo umekuwa ukiwakosesha watu wa Neno kwa muda mrefu huduma muhimu zikiwemo za afya na elimu.

“Huu ni mradi muhimu kwetu, na tunashukuru sana. Tunataka kuihakikishia kampuni ya CR20 kuwa ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na ofisi zote za serikali na jumuiya za mitaa, tutashirikiana kutoa uungaji mkono wote muhimu hadi mradi utakapokamilika", Mpinga amesema.

Mradi huo wa Barabara ya Neno-Ligowe unahusisha kuboresha barabara ya udongo iliyopo, ambayo mara nyingi huwa haipitiki, hadi kuwa barabara ya lami yenye upana wa mita 9.5. Barabara hiyo ni muhimu kwa usafiri na maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika eneo hilo, ikiunganisha Mwanza, kituo kikuu cha mpakani, hadi Ntcheu, kitovu cha biashara ya mazao ya kilimo katikati mwa Malawi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Deng Jie)

Picha