Rais Xi Jinping asema China na Russia zimepata njia sahihi ya ujirani mwema kwa nchi jirani kubwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 23, 2024

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Russia Vladimir Putin  huko Kazan, Russia, Oktoba 22, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Russia Vladimir Putin huko Kazan, Russia, Oktoba 22, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)

KAZAN, Russia - Rais wa China Xi Jinping jana siku ya Jumanne alipokutana na Rais wa Russia Vladimir Putin alisema kuwa China na Russia zimepata njia sahihi ya kuwa na ujirani mwema kwa nchi kubwa jirani, njia hiyo ni kutofungamana na upande wowote, kutopambana na kutolenga upande wowote wa tatu.

Rais Xi amesema kuwa mwaka huu ni mwaka wa 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Russia, na katika miaka hiyo mingi iliyopita uhusiano kati ya nchi hizo mbili umepita na kushinda nyakati mbalimbali za changamoto.

Rais Xi amesema, pande zote mbili zinashikilia moyo wa ujirani mwema na urafiki wa kudumu, uratibu wa kimkakati wa pande zote, na ushirikiano wa kunufaishana wa kupata maendeleo kwa pamoja, zimeendeleza kwa kina na kupanua uratibu wao wa kimkakati wa pande zote na ushirikiano wenye matokeo halisi katika sekta mbalimbali, Rais Xi amesema.

Rais Xi akieleza kuwa Dunia leo inakabiliwa na mabadiliko makubwa ambayo hayajapata kuonekana katika miaka 100 iliyopita, yakisababisha mabadiliko ya haraka ya hali yakimataifa na kuleta misukosuko, na ameelezea imani yake kuwa urafiki mkubwa na wa kudumu kati ya China na Russia hautabadilika, na zikiwa nchi kubwa, hisia zao za kuwajibika kwa Dunia na kwa watu hazitabadilika pia.

Rais Xi amesisitiza, Mwaka ujao ni maadhimisho ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa (UN) na ushindi wa Vita vya Dunia vya Kupambana na Ufashisti, China na Russia, zote ni nchi wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la UN na nchi kubwa duniani, zinapaswa kuzidisha uratibu wa kimkakati wa pande zote, kuimarisha mawasiliano na uratibu ndani ya mifumo ya ushirikiano wa pande nyingi kama vile Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO), kuhimiza mtazamo sahihi wa historia ya Vita vya Pili vya Dunia, kulinda kithabiti mfumo wa kimataifa ambao kiini chake ni Umoja wa Mataifa, na kulinda kwa pamoja utulivu wa kimkakati wa dunia nzima na haki na usawa wa kimataifa,.

Rais Putin amesema, mwaka ujao ni mwaka wa 80 tangu kumalizika kwa Vita vya Pili vya Dunia, Russia na China zilijitoa mhanga sana kwa ajili ya ushindi katika Vita vya Dunia vya Kupambana na Ufashisti, na Russia inapenda kuadhimisha pamoja na China mnara huu muhimu wa kihistoria.

Russia pia inapenda kudumisha mawasiliano ya karibu ya ngazi ya juu na uratibu wa kimkakati na China katika mambo ya kimataifa, na kushirikiana na China katika kulinda haki na usawa wa kimataifa pamoja na utulivu wa kimkakati wa dunia nzima, ameongeza Rais Putin.

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Russia Vladimir Putin huko Kazan, Russia, Oktoba 22, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Russia Vladimir Putin huko Kazan, Russia, Oktoba 22, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)

Picha