

Lugha Nyingine
Jeshi la Israel lathibitisha kuuawa kwa kiongozi wa Hezbollah Hashem Safieddine
(CRI Online) Oktoba 23, 2024
Jeshi la Israel limethibitisha kuwa Hashem Safieddine, mkuu wa Baraza Tendaji la kundi la Hezbollah, aliuawa katika shambulizi la anga mjini Beirut wiki tatu zilizopita.
Safieddine aliuawa katika shambulizi la bomu lililofanywa na ndege za kivita za Israel kwenye kitongoji cha kusini mwa Beirut, jeshi la Israel limesema, likiongeza kuwa shambulizi hilo lililenga jengo yalipo makao makuu ya kijasusi ya chini ya ardhi ya Hezbollah.
Jeshi hilo limesema makamanda waandamizi 25 wa Hezbollah walikuwepo kwenye jengo hilo wakati wa shambulizi hilo, lakini halikufafanua kama walinusurika au la.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma