

Lugha Nyingine
Zaidi ya asilimia 94 ya Watanzania wajiandikisha kwenye daftari la wapiga kura
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 23, 2024
Waziri wa nchi katika Ofisi ya Rais anayeshughulikia mambo ya utawala wa mikoa na serikali za mitaa wa Tanzania Bw. Mohamed Mchengerwa amesema kuanzia tarehe 11 hadi tarehe 22 Oktoba, watanzania wasiopungua 31,282,331 wamejiandikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba, ikiwa ni sawa na asilimia 94.83 ya Watanzania wenye haki ya kupiga kura. Kati ya Watanzania waliojiandikisha, asilimia 48.71 ni wanaume huku asilimia 51.29 ni wanawake.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mikoa yote 26 ya Tanzania imefanya kazi vizuri katika kuwaandikisha wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi huo.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Deng Jie)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma