Lugha Nyingine
Uchumi wa kidijitali wa Kenya katika mwelekeo wa kukua kutokana na motisha ya kiudhibiti: ripoti
Uchumi wa kidijitali wa Kenya utadumisha kasi ya ukuaji katika siku za usoni, ukichochewa na motisha za kisera na kiudhibiti, uvumbuzi unaoongozwa na vijana, na kuongezeka kwa mtiririko wa mtaji, imeeleza ripoti, iliyotolewa mjini Nairobi, Kenya jana Jumanne.
Ripoti hiyo yenye jina la “Kuchochea Mageuzi ya Kidijitali ya Uchumi nchini Kenya” iliyokusanywa matokeo yake na “Global System for Mobile Communications Association” (GSMA) na washirika wake, inaonyesha kuwa uchumi wa kidijitali utachangia karibu dola bilioni 5.13 za Marekani kwenye pato la taifa la Kenya ifikapo mwaka 2028.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo, waziri wa habari, mawasiliano na uchumi wa kidijitali wa Kenya, Bibi Margaret Ndung'u, amesema kuendeleza mambo ya kidijitali kunashikilia ufunguo wa ukuaji endelevu, uundaji wa nafasi za ajira, utoaji wa huduma bora, na ongezeko la mapato ya Kenya.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma