Xi azitaka China na India kuhimizana katika kutimiza matarajio ya maendeleo ya kila upande, atoa wito kwa China na India kuwezeshana kutafuta maendeleo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 24, 2024

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi  katika wakati wa Mkutano wa 16 wa Viongozi wa BRICS  huko Kazan, Russia, Oktoba 23, 2024. (Xinhua/Shen Hong)

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi katika wakati wa Mkutano wa 16 wa Viongozi wa BRICS huko Kazan, Russia, Oktoba 23, 2024. (Xinhua/Shen Hong)

KAZAN, Russia - Rais Xi Jinping wa China jana Jumatano alipokutana na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi katika wakati wa Mkutano wa 16 wa Viongozi wa nchi za BRICS alitaka China na India kuimarisha mawasiliano na ushirikiano, kuongeza hali ya kuaminiana kimkakati, na kuhimizana katika kutafuta matarajio ya maendeleo.

Rais Xi amesema China na India zikiwa nchi zenye ustaarabu wa historia ndefu, nchi kubwa zinazoendelea na sehemu muhimu ya Nchi za Kusini, nchi hizo mbili ziko kwenye kipindi muhimu cha mchakato wa ujenzi wa mambo ya kisasa.

Xi amesema, kufuata mkondo wa historia na mwelekeo sahihi wa uhusiano wa pande mbili kunalingana na maslahi ya kimsingi ya nchi hizo mbili na watu wao, akizihimiza pande hizo mbili kubeba wajibu wao wa kimataifa, kuweka mfano wa kuigwa, kuimarisha nguvu na mshikamano wa nchi zinazoendelea, na kuchangia katika kuhimiza dunia yenye ncha nyingi na demokrasia zaidi katika uhusiano wa kimataifa.

Amesisitiza kuwa uhusiano kati ya China na India kimsingi ni suala la namna zinavyotendeana kati ya nchi hizo mbili kubwa zinazoendelea na majirani, ambazo kila moja ina idadi ya watu bilioni 1.4.

Xi amesema, maendeleo sasa ndiyo lengo kubwa zaidi la pamoja la China na India, pande hizo mbili zinapaswa kuendelea kushikilia maoni yao muhimu ya pamoja, ikiwa ni pamoja na kwamba China na India kila upande ni fursa ya maendeleo wala si tishio kwa upande mwingine, na ni washirika wa ushirikiano wala si washindani.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Modi, ameeleza kuwa kudumisha ukuaji tulivu wa uhusiano kati ya India na China ni muhimu sana kwa nchi hizo mbili na watu wake. Amesema siyo tu kwamba umuhimu huu unahusiana na ustawi na mustakabali wa watu bilioni 2.8, bali pia ni umuhimu mkubwa kwa amani utulivu wa kanda na hata Dunia kwa ujumla.

Viongozi hao wawili wamepongeza maendeleo muhimu ya pande hizo mbili hivi karibuni kupitia mawasiliano ya mara kwa mara juu ya kutatua masuala husika katika maeneo ya mpakani. Waziri Mkuu Modi ametoa mapendekezo kadhaa juu ya kuboresha na kuendeleza uhusiano kati ya India na China, ambayo Rais Xi ameyakubali kikanuni.

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi  katika wakati wa Mkutano wa 16 wa Viongozi wa BRICS huko Kazan, Russia, Oktoba 23, 2024. (Xinhua/Shen Hong)

Rais Xi Jinping wa China akikutana na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi katika wakati wa Mkutano wa 16 wa Viongozi wa BRICS huko Kazan, Russia, Oktoba 23, 2024. (Xinhua/Shen Hong)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha