Lugha Nyingine
Rais Xi akutana na mwenzake wa Misri El-Sisi
Rais Xi Jinping wa China amekutana na mwenzake wa Misri Abdel Fattah El-Sisi Jumatano usiku pembezoni mwa Mkutano wa 16 wa Viongozi wa nchi za BRICS uliofanyika mjini Kazan, Russia.
Rais Xi ameipongeza na kuikaribisha Misri kushiriki kwa mara ya kwanza katika mkutano huo wa viongozi wa nchi za BRICS kama mwanachama rasmi.
Rais Xi amebainisha kuwa huu ni mwaka wa kumi tangu China na Misri zianzishe uhusiano wa washirika wa kimkakati wa pande zote, akisema China inaiunga mkono kithabiti Misri kulinda mamlaka, usalama na maslahi yake ya maendeleo, na ina nia ya kuwa rafiki wa dhati na mshirika wa karibu wa maendeleo wa Misri.
Kwa upande wake Rais El-Sisi amesema katika muongo uliopita tangu Misri na China zilipoanzisha uhusiano wa washirika wa kimkakati wa pande zote, nchi hizo mbili zimepata matunda mengi ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali.
Ameishukuru China kwa kuiunga mkono Misri kujiunga na BRICS, na kwamba Misri ina nia ya kushirikiana kwa karibu na China katika kulinda maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea na Nchi za Kusini, na kusukuma mbele ujenzi wa mfumo wa utawala wa dunia ulio wa haki na usawa zaidi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma