Lugha Nyingine
China yatangaza orodha ya miradi ya uwekezaji yenye thamani ya Yuan bilioni 200
Picha hii iliyopigwa tarehe 17 Oktoba 2024 ikionyesha eneo la ujenzi wa stesheni ya jumuishi ya usafiri wa umma katika Eneo la Tongzhou, mjini Beijing, mji mkuu wa China. (Xinhua/Ju Huanzong)
BEIJING - China imetangaza orodha ya miradi yenye thamani ya yuan bilioni 200 (dola kama bilioni 28 za Kimarekani) ambayo iko katika mipango ya uwekezaji ya mwaka ujao, ofisa wa Kamati Taifa ya Maendeleo na Mageuzi ya China (NDRC) ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua Jumanne.
Miradi hiyo 647 ya uwekezaji iliyotangaza mapema kwa utangulizi mwaka huu ni pamoja na mitandao ya mabomba ya mijini chini ya ardhi, kutumia ajira kama njia ya kupunguza maafa, kuimarisha hifadhi zilizochakaa, uhifadhi na urejeshaji wa ikolojia, miundombinu ya usafirishaji, maeneo muhimu ya umma kama vile elimu, afya na utamaduni, vilevile maeneo muhimu ya kuhifadhi mazao ya kilimo, afisa huyo wa NDRC.
NDRC itasonga mbele na kuanzisha na kutekeleza miradi hiyo haraka iwezekanavyo, amesema afisa huyo, akiongeza kuwa juhudi zitafanywa kufikia maendeleo halisi mwaka huu ili kutoa uungaji mkono mkubwa kwa ukuaji wa uchumi katika robo ya nne ya mwaka huu.
Afisa huyo amesema kuwa msingi wa kufikia lengo la ukuaji wa uchumi la mwaka mzima ni thabiti kabisa, akitaja sababu zinazofaa kama vile kasi ya mwelekeo wa kuongezeka kwa data muhimu kwa Oktoba na kiwango cha ukuaji wa Pato la Taifa cha asilimia 4.8 katika robo tatu za kwanza.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma