

Lugha Nyingine
Mkutano wa Kuzalisha na Kuchangia Maudhui ya “Fursa za China kwa Vyombo vya Habari vya Asia-Pasifiki Kutembelea Guizhou” wafanyika Guiyang
Mkutano wa Kuzalisha na Kuchangia Maudhui ya “Fursa za China kwa Vyombo vya Habari vya Asia-Pasifiki Kutembelea Guizhou”umefanyika katika Mji wa Guiyang, Mkoa wa Guizhou, China, siku ya Jumanne, Oktoba 22.
Kwenye mkutano huo, wakuu wa idara husika kama vile Idara ya Uenezi ya Kamati ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Mkoa wa Guizhou, Idara ya Elimu ya Mkoa wa Guizhou, Idara ya Ikolojia na Mazingira ya Mkoa wa Guizhou, Idara ya Utamaduni na Utalii ya Mkoa wa Guizhou, Ofisi ya Data Kubwa ya Mkoa wa Guizhou na waandishi wa habari 17 kutoka nchi 15 za eneo la Asia-Pasifiki walikusanyika pamoja na kuchangia uzoefu wao wa maisha na sifa za utamaduni wa nchi au maeneo yao, vilevile mambo ambayo wameona, kusikia, na kufikiria wakati wa safari yao ya Guizhou.
Ili kueneza sauti ya China na kusimulia vizuri simulizi ya Guizhou kwenye jukwaa la kimataifa, mradi wa Gazeti la Mtandaoni la People's Daily wa Mawasiliano ya Kirafiki ya Vijana wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" - "Fursa za China kwa·Vyombo vya Habari vya Asia-Pasifiki Kutembelea Guizhou" wenye maudhui maalum ya safari hiyo ulizinduliwa rasmi.
Katika siku saba za shughuli hiyo, waandishi wa habari kutoka Malaysia, Thailand, Indonesia na nchi na maeneo mengine watatembelea Mji wa Guiyang, Eneo linalojiendesha la Makabila ya Wamiao na Wadong la Mashariki-Kusini mwa Mkoa wa Guizhou na Mji wa Bijie ili kujionea mafanikio ya maendeleo ya Guizhou.
Picha ikionyesha hali ya mkutano huo. (Picha na Liu Yang)
Picha ikionyesha hali ya mkutano huo. (Picha na Liu Yang)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma