Sekta ya viwanda ya China yaendelezwa vizuri katika robo tatu za kwanza mwaka huu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 24, 2024

Picha hii iliyopigwa tarehe 25 Aprili 2024 ikionyesha gari linalotumia nishati mpya (NEV) lililozalishwa na BYD, kampuni ongozi ya China kwa kuzalisha NEV, katika kiwanda cha BYD mjini Zhengzhou, Mkoa wa Henan, katikati mwa China. (Xinhua/Li Jianan)

Picha hii iliyopigwa tarehe 25 Aprili 2024 ikionyesha gari linalotumia nishati mpya (NEV) lililozalishwa na BYD, kampuni ongozi ya China kwa kuzalisha NEV, katika kiwanda cha BYD mjini Zhengzhou, Mkoa wa Henan, katikati mwa China. (Xinhua/Li Jianan)

BEIJING - Sekta ya viwanda ya China imepata ukuaji thabiti katika robo tatu za kwanza Mwaka 2024, Wizara ya Viwanda na Teknolojia ya Habari ya China imesema Jumatano ambapo viwanda vya kutengeneza vifaa na vya teknolojia ya hali ya juu vinakua kwa kasi.

Viwanda kama vile vya kielektroniki, madini yasiyo metali, kemikali na magari vilichukua karibu nusu ya ukuaji wa uzalishaji wa viwandani ulioshuhudiwa katika robo tatu za kwanza, wizara hiyo imesema.

Katika kipindi hicho, pato la ongezeko la thamani la sekta ya magari liliongezeka kwa asilimia 7.9 mwaka hadi mwaka, takwimu za wizara hiyo zinaonyesha.

Kufuatia kuungwa mkono kwa mpango wa biashara ya kubadilisha bidhaa za walaji nchini China, mauzo ya bidhaa za kielektroniki na kidijitali yameongezeka sana.

Kuanzia Januari hadi Septemba, pato la ongezeko la thamani la kampuni katika sekta ya uzalishaji wa vifaa vya elektroniki za China zenye mapato makuu ya biashara ya kila mwaka ya angalau yuan milioni 20 (kama dola milioni 2.81 za Kimarekani) yaliongezeka kwa asilimia 12.8 mwaka hadi mwaka.

Idadi ya simu janja zilizouzwa katika soko la ndani ilifikia milioni 220, ikiwa ni ongezeko la asilimia 9.9 kutoka kipindi kama hicho mwaka jana, takwimu hizo zinaonyesha.

China pia imeeendelea kuboresha muundo wake wa viwanda. Uzalishaji na uuzaji wa magari yanayotumia nishati mpya uliongezeka kwa asilimia 31.7 na asilimia 32.5 mtawalia, na China ilichukua zaidi ya asilimia 70 ya oda zote duniani za kuunda meli kwa teknolojia za kijani.

Katika miezi minane ya kwanza, kiwango cha mapato ya uendeshaji wa kampuni "ndogo zenye nguvu" za China ambazo zina mapato ya biashara ya angalau yuan milioni 20 kwa mwaka yalikuwa asilimia 7.5 - juu ya kiwango cha wastani cha kampuni za viwanda, wizara hiyo imesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha