FAO yatoa wito wa kuongezwa fedha ili kukabiliana na uhaba wa chakula nchini Botswana

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 24, 2024

Carla Mucavi, mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) nchini Botswana, akizungumza kwenye shughuli ya kuadhimisha Siku ya Chakula Duniani mjini Gaborone, Botswana, Oktoba 22, 2024. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

Carla Mucavi, mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO) nchini Botswana, akizungumza kwenye shughuli ya kuadhimisha Siku ya Chakula Duniani mjini Gaborone, Botswana, Oktoba 22, 2024. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

GABORONE – Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limetoa wito wa kuongezwa fedha na suluhu zenye uvumbuzi ili kukabiliana na uhaba wa chakula unaosababishwa na hali ya ukame nchini Botswana na kuhakikisha usalama wa chakula.

Carla Mucavi, mwakilishi wa FAO nchini Botswana, amesema Jumanne kwenye shughuli ya kuadhimisha Siku ya Chakula Duniani huko Gaborone, mji mkuu wa nchi hiyo kwamba watu takriban 37,000 nchini Botswana wanakabiliwa na uhaba wa chakula kutokana na hali ya ukame wa muda mrefu, huku akieleza kuwa duniani kote, watu karibu milioni 733 wana utapiamlo.

Mucavi amesisitiza kuwa Ripoti ya Kamati ya Tathmini ya Matatizo ya Botswana Mwaka 2024 inabainisha hitaji la dharura la kuongezeka kwa ufadhili. Ametoa wito wa suluhu yenye uvumbuzi ya mambo ya fedha, kama vile fedha za hisani na mikopo yenye masharti nafuu, ili kuziba pengo la ufadhili na kuimarisha uhimilivu dhidi ya changamoto kama vile mabadiliko ya tabianchi na kuyumba kwa uchumi.

Katika juhudi zake za kuisaidia Botswana katika kukabiliana na njaa, utapiamlo na uharibifu wa ardhi, FAO imeidhinisha miradi minne mipya ya kuunga mkono ufugaji wa samaki, uzalishaji wa malisho ya mifugo, programu za kulisha wanafunzi shuleni, na mpango wa Mji wa Kijani. Amesema, miradi hiyo imepata ufadhili na inatarajiwa kuanza kutekelezwa mnamo 2025.

Wakati huo huo, serikali ya Botswana ilizindua mpango wa kilimo wenye thamani ya mamilioni ya dola za Marekani mwezi Aprili kuboresha ustawi wa jamii huku ikifikia malengo ya taifa ya usalama wa chakula na lishe.

Siku ya Chakula Duniani, ambayo inaadhimishwa kila mwaka tarehe 16 Oktoba, ilianzishwa na FAO Mwaka 1945 ili kuongeza ufahamu wa watu kuhusu njaa na changamoto za usalama wa chakula.

Watu wakishiriki kwenye shughuli ya kuadhimisha Siku ya Chakula Duniani mjini Gaborone, Botswana, Oktoba 22, 2024. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

Watu wakishiriki kwenye shughuli ya kuadhimisha Siku ya Chakula Duniani mjini Gaborone, Botswana, Oktoba 22, 2024. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha