Wataalamu wa Ethiopia wapongeza njia ya ujenzi wa mambo ya kisasa ya China kuwa kichocheo muhimu kwa maendeleo ya dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 24, 2024

Wataalamu na maofisa wa China na Ethiopia wakifanya majadiliano ya wanajopo kwenye mazungumzo ya ngazi ya juu ya kunufaika pamoja uzoefu mjini Addis Ababa, Ethiopia, tarehe 22 Oktoba 2024. (Xinhua/Habtamu Worku)

Wataalamu na maofisa wa China na Ethiopia wakifanya majadiliano ya wanajopo kwenye mazungumzo ya ngazi ya juu ya kunufaika pamoja uzoefu mjini Addis Ababa, Ethiopia, tarehe 22 Oktoba 2024. (Xinhua/Habtamu Worku)

ADDIS ABABA - Wataalamu wa Ethiopia kwenye mazungumzo ya ngazi ya juu ya kunufaika pamoja uzoefu yaliyofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia, Jumanne wamepongeza njia ya China ya Ujenzi wa Mambo ya Kisasa kuwa ni kichocheo muhimu kwa maendeleo na upigaji hatua wa Dunia, haswa katika kuhimiza mfumo wa kimataifa wenye pande nyingi na uwiano zaidi.

Melaku Mulualem, mtafiti mwandamizi wa uhusiano wa kimataifa na diplomasia katika Taasisi ya Mambo ya Nje ya Ethiopia, amesema kuwa ujenzi wa mambo ya kisasa, kwa China, si tu kuhusu maendeleo ya kiuchumi, bali pia kuboresha maisha ya watu.

Mtafiti huyo amesema China iliweza kuandaa njia yake ya ujenzi wa mambo ya kisasa kwa kuendana na hali yake yenyewe, ambapo mageuzi na ufunguaji mlango ndiyo msingi wa safari yake hiyo ya ujenzi wa mambo ya kisasa.

"China kujiendeleza kuwa nchi ya kisasa kunatokana na msukumo wa ndani na kunaendana na mazingira ya China. Ni ujenzi wa mambo ya kisasa wa maendeleo ya amani. Ujenzi wa mambo ya kisasa wa China unajumuisha watu wote na unazingatia maslahi ya watu. Ni ujenzi wa mambo ya kisasa wa mapatano kati ya binadamu na mazingira ya asili," Mulualem amesema kwenye mazungumzo hayo chini ya mada ya "Fursa Mpya kwa Ushirikiano wa China na Ethiopia katika Juhudi za Pamoja za Ujenzi wa Mambo ya Kisasa".

Akielezea njia ya China ya ujenzi wa mambo ya kisasa kuwa "mfano wa kuigwa," hasa kwa nchi zilizoko nyuma kimaendeleo duniani, Mulualem amesisitiza haja muhimu ya kuhimiza na kupanua kanuni asilia, ujuzi na ustadi wa maendeleo ya China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha