Wafanyabiashara wa Zimbabwe watafuta fursa katika maonesho ya CIIE Shanghai

(CRI Online) Oktoba 24, 2024

Clive Chirova, mkurugenzi wa kampuni ya Samuneti Leathers ambayo ni mtengenezaji bidhaa bora za ngozi amesema Maonesho ya Kimataifa ya Uagizaji Bidhaa ya China (CIIE) yametoa jukwaa kwa kufungua fursa za kibiashara kwa sekta ya bidhaa za sanaa ya Zimbabwe.

Maonesho hayo yatakayofanyika huko Shanghai, mashariki mwa China kuanzia Novemba 5 hadi 10, ni moja kati ya maonesho makubwa zaidi ya kimataifa ya uagizaji bidhaa duniani yakilenga kufungua soko la China kwa nchi za kigeni.

Chirova amesema, jukwaa hilo la kimataifa linaiwesesha kampuni hiyo kupanua mauzo yake ya bidhaa.

Amesema wanatakiwa kupanua mauzo yao yanayotokana na ukuaji wa sekta ya ngozi pamoja na bidhaa nyingine.

Ameongeza kuwa kufunguliwa kwa soko kubwa la China kwa sekta ya bidhaa za sanaa ya Zimbabwe, kumeleta fursa nyingi kwa kampuni za nchi yake kutafuta kupanua biashara zao katika masoko ya China na kimataifa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha