Xi Jinping atoa sauti ya kuunga mkono Nchi za Kusini katika siku ya mwisho ya mkutano wa viongozi wa BRICS wa Kazan

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 25, 2024

Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba muhimu yenye kichwa "Kuunganisha Nguvu Kubwa ya Nchi za Kusini Kujenga Pamoja Jumuiya ya Binadamu yenye Mustakabali wa Pamoja" kwenye mazungumzo ya viongozi wa nchi za "BRICS Plus"  huko Kazan, Russia, Oktoba 24, 2024. (Xinhua/Li Xueren)

Rais Xi Jinping wa China akitoa hotuba muhimu yenye kichwa "Kuunganisha Nguvu Kubwa ya Nchi za Kusini Kujenga Pamoja Jumuiya ya Binadamu yenye Mustakabali wa Pamoja" kwenye mazungumzo ya viongozi wa nchi za "BRICS Plus" huko Kazan, Russia, Oktoba 24, 2024. (Xinhua/Li Xueren)

KAZAN, Russia - Wakati viongozi wa nchi za BRICS walipokutana na nchi zisizo wanachama zinazotafuta uhusiano wa karibu na jumuiya hiyo siku ya Alhamisi, Rais wa China Xi Jinping ameeleza uungaji mkono mkubwa kwa Nchi za Kusini wakati akishiriki kwenye mazungumzo ya viongozi wa nchi za "BRICS Plus" siku ya mwisho ya mkutano huo wa Kazan.

Rais Xi amesema “kuibuka kwa pamoja kwa Nchi za Kusini ni umaalum wazi wa mageuzi makubwa duniani kote”

"Tunaunga mkono nchi zaidi za Kusini katika kujiunga na mambo ya nchi za BRICS zikiwa wanachama rasmi, nchi washirika au nchi za 'BRICS Plus' ili tuweze kuunganisha nguvu kubwa ya Nchi za Kusini kujenga pamoja jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja," Rais Xi amesema.

Rais huyo wa China amesema, Haijalishi jinsi hali ya kimataifa inavyobadilika, "sisi nchini China daima tutaziweka Nchi za Kusini mioyoni mwetu, na kudumisha mizizi yetu katika Nchi za Kusini."

Viongozi kutoka Asia, Afrika, Mashariki ya Kati na Latini Amerika, vilevile na wajumbe wa mashirika kadhaa ya kimataifa, walihudhuria mkutano huo akiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Ajenda ya Mkutano wa 16 wa Viongozi wa nchi za BRICS ilihusisha masuala kadhaa muhimu, ikiwa ni pamoja na amani na utulivu duniani, mageuzi ya usimamizi wa dunia , maendeleo endelevu, kutokomeza umaskini, mabadiliko ya tabianchi, na mapambano dhidi ya ugaidi na uhalifu wa kuvuka mipaka.

Rais wa Russia Vladimir Putin aliyeendesha mkutano huo, amesema ni muhimu kwa nchi wanachama wa BRICS kujadili masuala haya yote na nchi za kutoka Kusini.

"Nchi zetu zote zinayo matarajio, maadili na maono ya utaratibu mpya wa dunia ulio wa kidemokrasia ambao unaakisi utamaduni na ustaarabu tofauti mbalimbali," Putin amesema.

Mkutano huo wa viongozi wa nchi za BRICS wa Kazan ni mkutano wa kwanza wa ana kwa ana wa viongozi wa nchi za BRICS baada ya kuongezwa nchi wanachama wa jumuiya hiyo mwaka jana. Siku ya Jumatano, viongozi hao wa nchi za BRICS walipitisha azimio la mkutano wa Kazan, ambalo lilifanya majumuisho ya matokeo ya mkutano huo. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha