Uchumi wa kimataifa hatarini kukwama kwenye njia ya ukuaji mdogo wenye deni kubwa: IMF

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 25, 2024

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Kristalina Georgieva akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Washington, D.C., Marekani, Oktoba 24, 2024. (Xinhua/Hu Yousong)

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Kristalina Georgieva akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Washington, D.C., Marekani, Oktoba 24, 2024. (Xinhua/Hu Yousong)

WASHINGTON - Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limeonya siku ya Alhamisi kwamba uchumi wa dunia uko katika hatari ya kukwama kwenye njia ya ukuaji mdogo wenye madeni makubwa, likitoa wito kwa watunga sera kuchukua hatua juu ya deni na kufanya mageuzi yenye kuunga mkono ukuaji wa uchumi.

"Uchumi wa dunia uko katika hatari ya kukwama kwenye njia ya ukuaji mdogo wenye madeni makubwa, hiyo ina maana mapato ya chini na ajira chache. Pia inamaanisha mapato ya chini ya serikali, hivyo uwekezaji mdogo kuunga mkono familia na kupambana na changamoto za muda mrefu kama vile mabadiliko ya tabianchi," Mkurugenzi Mkuu wa IMF Kristalina Georgieva amesema katika mkutano na waandishi wa habari kwenye Mikutano ya Mwaka ya IMF na Benki ya Dunia Mwaka 2024 inayoendelea.

Kwanza, Georgieva ametoa wito kwa watunga sera kuhakikisha kwamba mfumuko wa bei unarudi kwenye lengo kila mahali, akibainisha kuwa mbinu sasa kwa benki kuu ni "kumaliza kazi ya mfumuko wa bei bila kulazimika kuharibu soko la ajira."

Pili, "sasa ni wakati wa kuchukua hatua juu ya deni na nakisi baada ya miaka mingi ya uungaji mkono uliohitajika sana wa seza za mambo ya fedha katika majaribio ya mwitikio. Sasa ni wakati wa kujenga upya nguzo imara za mambo ya fedha katika nchi nyingi. Hilo linaweza kufanyika hatua kwa hatua, lakini inahitaji kuanza sasa," ameendelea kusema.

Tatu na muhimu zaidi, amesema, ni muhimu kwamba nchi zifanye mageuzi yanayounga mkono ukuaji wa uchumi kuanzia kupunguza urasimu hadi kuboresha usimamizi, akibainisha kuwa uchambuzi wa IMF unaonyesha kuwa mageuzi haya yanaweza kuongeza pato kwa asilimia 8 katika kipindi cha miaka minne katika nchi zinazoendelea.

Kwenye ripoti ya Mtazamo mpya wa Uchumi wa Dunia (WEO) iliyotolewa Jumanne, IMF ilidumisha makadirio yake ya ukuaji wa kimataifa Mwaka 2024 kwa asilimia 3.2, kulingana na makadirio yake ya awali ya mwezi wa Julai. Matarajio ya ukuaji wa uchumi kwa miaka mitano kuanzia sasa yameendelea kuwa duni, katika asilimia 3.1, ikiwa ni kiwango cha chini zaidi katika miongo kadhaa.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Kristalina Georgieva akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Washington, D.C., Marekani, Oktoba 24, 2024. (Xinhua/Hu Yousong)

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Kristalina Georgieva akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Washington, D.C., Marekani, Oktoba 24, 2024. (Xinhua/Hu Yousong)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha