

Lugha Nyingine
Rais wa Zimbabwe ataka vikwazo vilivyowekwa na Marekani dhidi ya nchi hiyo viondolewe
(CRI Online) Oktoba 25, 2024
Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amezishukuru nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) kwa uungaji mkono wao katika wito wa Zimbabwe wa kutaka vikwazo vilivyowekwa na Marekani na washirika wake zaidi ya miongo miwili iliyopita dhidi ya nchi hiyo viondolewe.
Rais Mnangagwa ametoa kauli hiyo kwenye hotuba yake kama mwenyekiti wa jumuiya hiyo kabla ya Siku ya Kupinga Vikwazo ya SADC, ambayo imekuwa ikiadhimishwa tarehe 25 Oktoba kila mwaka tangu mwaka 2019, ili kupinga vikwazo hivyo vilivyowekwa dhidi ya Zimbabwe.
Rais Mnangagwa amesema vikwazo hivyo vimedhoofisha juhudi za pamoja kuelekea utangamano na maendeleo endelevu ya kikanda.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma