

Lugha Nyingine
Kenya yaahidi kuimarisha ulinzi wa wanyama wala nyama wakati tishio dhidi yao likiongezeka
(CRI Online) Oktoba 25, 2024
Kenya itaongeza juhudi zinazolenga kulinda wanyama wala nyama wakiwemo Simba, fisi wenye madoa na chui, wakati tishio dhidi ya wanyama hao likiendelea kuongezeka.
Akizungumza kwenye mkutano wa 14 kuhusu wanyama hao unaofanyika mjini Nairobi, mkurugenzi mkuu wa Shirika la Huduma za Wanyamapori la Kenya (KWS) Bw. Erustus Kanga, amesema kulinda wanyama hao katika makazi yao ya asili ni muhimu katika kuendeleza mapato ya utalii na uwiano wa ikolojia.
Bw. Kanga amesema idadi ya wanyama hao nchini Kenya imekuwa ikipungua kutokana na mshtuko wa mabadiliko ya tabia nchi, uharibifu wa makazi yao, kupungua kwa mawindo yao, na mashambulizi ya kulipiza kisasi yanayofanywa na jamii za wafugaji.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma