Faida ya viwanda vya China yafikia yuan zaidi ya trilioni 5 katika robo tatu za kwanza mwaka huu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 28, 2024

Mfanyakazi akiwa kazini kwenye mstari wa uzalishaji wa kiwanda cha Kampuni ya Teknolojia za Kiviwanda ya Tianrun, iliyopo Wendeng, Mjini Weihai, Mkoani Shandong, Mashariki mwa China, Julai 21, 2023. (Xinhua/Guo Xulei)

Mfanyakazi akiwa kazini kwenye mstari wa uzalishaji wa kiwanda cha Kampuni ya Teknolojia za Kiviwanda ya Tianrun, iliyopo Wendeng, Mjini Weihai, Mkoani Shandong, Mashariki mwa China, Julai 21, 2023. (Xinhua/Guo Xulei)

BEIJING - Idara ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) Jumapili ilisema katika kipindi kati ya Januari hadi Septemba, faida ya jumla ya kampuni kubwa za viwanda nchini China imefikia yuan trilioni 5.23 (dola bilioni 735.41 za Kimarekani), ikiwa imepungua kwa asilimia 3.5 kwa mwaka.

Lakini viwanda vipya vinavyokua kwa kasi vikiwakilishwa na utengenezaji bidhaa za teknolojia ya hali ya juu vimekuwa na ukuaji wa haraka. Mtakwimu wa NBS Yu Weining amesema hali hiyo inadhihirisha uhimilivu wa maendeleo ya uchumi wa viwanda ya China.

Bw. Yu amesema kuna mambo mengi yaliyochangia kupungua kwa viwango vya ukuaji wa faida, ikiwa ni pamoja na ongezeko kubwa la msingi linganifu kwa mwaka tangu mwezi Agosti, mahitaji yasiyotosha kuleta ufanisi, na kushuka kwa bei ya bidhaa za viwandani. Mwezi wa Septemba pekee, faida ilipungua kwa asilimia 27.1 kwa mwaka.

NBS imesema faida ya jumla ya kampuni kubwa za viwanda iliongezeka kwa yuan bilioni 575.43 kuanzia Januari hadi Septemba ikilinganishwa na kipindi cha kuanzia Januari hadi Agosti.

Katika kipindi cha miezi tisa ya kwanza mwaka huu, faida za viwanda vya uzalishaji wa bidhaa za teknolojia ya hali ya juu iliongezeka kwa asilimia 6.3 kwa mwaka ikihimizwa na ongezeko la haraka la uzalishaji.

Yu amesema kiwango hicho cha ukuaji ni asilimia 9.8 zaidi ya kiwango cha wastani cha kampuni kubwa za viwanda, kikichangia asilimia 1.1 ya ukuaji wa faida kwa ujumla.

Kutokana na juhudi thabiti za kupanua mahitaji ya ndani, kuhamasisha matumizi, na kuleta utulivu wa mahitaji ya soko la kimataifa, faida ya sekta ya viwanda vya bidhaa za walaji iliongezeka kwa asilimia 2.4 kwa mwaka katika kipindi cha Januari-Septemba, ikichangia asilimia 0.5 ya ukuaji wa jumla wa faida ya viwanda.

Bw. Yu pia amesema uhimilivu wa vichocheo vipya vya ukuaji wa viwanda unaonekana, licha ya kupugungua kwa kiwango cha ukuaji wa faida ya viwanda, lakini kutokana na utulivu wa matarajio ya kampuni za viwanda na kuongezeka kwa imani, ukuaji wa faida ya viwanda unatarajiwa kurejea.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha