Bandari lango la China kuelekea ASEAN yashuhudia ongezeko la kasi la mauzo ya nje ya vipuri vya magari ya NEV

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 28, 2024

Picha iliyopigwa Oktoba 24, 2024 ikionyesha meli ya kontena iliyobeba vipuri vya magari yanayotumia nishati mpya (NEV) kwenye Bandari ya Qinzhou, Mkoani Guangxi, Kusini mwa China. (Xinhua/Zhang Ailin)

NANNING - Bandari ya Qinzhou, bandari lango la China kuelekea Jumuiya ya Nchi za Asia Kusini-Mashariki (ASEAN), imeshuhudia ongezeko la mara 70 la mauzo ya vipuri vya magari yanayotumia nishati mpya (NEV) katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Kundi la Kampuni za Reli la China, Tawi la Nanning.

Takwimu zinaonyesha kuwa, hadi kufikia Oktoba 22, kontena 11,370 za TEU zilizobeba vipuri vya NEV kutoka Liuzhou, mji wa nchi kavu barani katika Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, kusini mwa China, zilikuwa zimesafirishwa kutoka Bandari ya Qinzhou mwaka huu, Kiasi ambacho kimeongezeka mara 70 ikilinganishwa na jumla ya kila mwaka ya kontena 160 za TEU Mwaka 2019.

Picha iliyopigwa Oktoba 24, 2024 ikionyesha treni ikiondoka kwenye Bandari ya Qinzhou, Mkoani Guangxi, kusini mwa China. (Xinhua/Zhang Ailin)

Picha iliyopigwa Oktoba 24, 2024 ikionyesha treni ikiondoka kwenye Bandari ya Qinzhou, Mkoani Guangxi, kusini mwa China. (Xinhua/Zhang Ailin)

Uuzaji nje wa vipuri vya magari wa Kampuni ya Magari ya SAIC-GM-Wuling (SGMW) ya Liuzhou, ambayo ni kampuni ya ubia kati ya SAIC Motor, General Motors na Liuzhou Wuling Motors, umepanuka kutoka masoko ya nchi za Asia Kusini-Mashariki hadi masoko ya nchi na maeneo zaidi ya 40, zikiwemo zile za Amerika ya Kati na Kusini na Mashariki ya Kati.

Ili kuhudumia vyema mahitaji ya usafirishaji ya kampuni za mkoani humo zinazozalisha NEV, mamlaka za reli zilianzisha huduma mpya zinazounganisha reli na bahari mwezi wa Julai mwaka huu ambapo treni mbili sasa zinaendeshwa mara kwa mara kila Jumatatu na Alhamisi, na kuokoa saa zaidi ya tano katika muda wa jumla wa usafirishaji ikilinganishwa na siku za nyuma.

Gari linalotumia nishati mpya (NEV) likijongea kwenye njia ya kiotomatiki katika kituo cha usambazaji mjini Liuzhou, Mkoani Guangxi, Kusini mwa China, Oktoba 23, 2024. (Xinhua/Zhang Ailin)

Gari linalotumia nishati mpya (NEV) likijongea kwenye njia ya kiotomatiki katika kituo cha usambazaji mjini Liuzhou, Mkoani Guangxi, Kusini mwa China, Oktoba 23, 2024. (Xinhua/Zhang Ailin)

Viwanda vya uzalishaji wa magari ya nishati mpya mji wa Liuzhou una tawisha, na magari madogo yenye rangi tofauti mji huo umekuwa turufu mpya ya kuvutia kwa mji huo.

Eneo la Bandari ya Qinzhou linajiimarisha kuwa bandari lenye ngazi ya juu ambalo linarahisisha usafirishaji wa mizigo kati ya China na ASEAN.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha